Serikali ya Urusi imetangaza kuidhinisha uamuzi wa kutaka kujitenga na mahakama kuu ya kimataifa.
Kulingana na maelezo yaliyotolewa na ikulu ya Kremlin, iliarifiwa kwamba rais Vladimir Putin ametia saini rasimu ya uamuzi huo wa kutaka kujitenga na mahakama kuu ya kimataifa kufuatia pendekezo la wizara ya sheria na masuala ya nje.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba Putin pia alitoa agizo la kuwasilishwa kwa uamuzi huo kwa ofisi ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitriy Peskov alifahamisha kuchukuliwa kwa uamuzi huo kutokana na vizuizi vya sheria vilivyopo kwa taifa la Urusi.
Wizara ya masuala ya nje ya Urusi pia ilikahsifu mahakama kuu ya kimataifa kwa ukosefu wa haki na uadilifu katika sheria kutokana na kushindwa kujitegemea.
Mahakama hiyo pia inadaiwa kuangazia mzozo wa Georgia wa mwaka 2008 kwa upande mmoja na kughadhabisha Urusi.