SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 14 Novemba 2016

T media news

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 39 & 40

Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA

Bwana Rusev aliendelea kutoa maelezo ya Hotel atakayo fikizia bwana Paul Henry Jr, akaonyesha kila sehemu ambayo bwana Paul Hery Jr atapita akiwa na watu wake wanao mlinda. Hadi mwisho wa maelekezo yake, wote wakawa wamemuelewa vizuri bwana Rusev.

“Agnes hii ni kazi yako ya kwanza na sinto hitaji ukosee, ninakuamini sana”

“Usijali mkuu nipo kwa ajili yako”      

“NITAHITAJI UMUUE KIONGOZI HUYU IWE TISHIO KWA NCHI HII NA DUNIA NZIMA”

“SAWA MKUU”

Agnes alijibu huku akiinamisha kichwa chake chini kama ishara ya kumuheshimu bwana Rusev, kisha bwana Rusev akachuku moja ya chini yenye alama ya X na kumvisha Agnes shingoni, akampa Baraka kwa ajili ya kuitekeleza kazi hiyo hatari sana kwa maisha yake.

                                                                                 

ENDELEA

Agnes akaanza kazi moja ya kulenga shabaha kwa masafa ya mbali pasipo kutumia lensi inayo saidia kuweza kuvuta vitu karibu, kila anacho kilenga kwa kutumia bunduki yake aina ya AS50 Sniper rifle, yenye uzito wa kila zaidi ya kumi na tano ikiwa na risasi zilizo jaa, akahakikisha anakipata vizuri huku akiwa ameishika mkononi mwake, jambo ambalo lilizidi kuwashangaza wengi kwani, hii ni bunduki ambayo mara nyingi mtu huwa anaiweka chini na kuisimamisha kupitia vimiguu viwili vya chuma, ili kuweza kulenga shaba.

“Waooooo”

Fetty alimpigia makofi Agens, baada ya kumkuta akiwa analenga vitu vya mbali kwa bunduki hiyo. Agnes baada ya kumuona Fetty akaacha zoezi lake ambalo analo kifanya

“Mwanangu kweli unatisha, hii ngoma ni nzito”

Fetty alizungumza huku akiinyanyua bundiki aliyo ishika Agnes

“Inahitaji mazoea kuweza kuitumia la sivyo unaweza ukafa, kwa maana ninapiga hadi nasikia mapigo ya moyo yanacheza kama kitenesi”

“Hahahaa, sas mtu wangu si uiweke chini ndio upige?”

“Ahaaa chini najiona kama nakosa shabaha vile”

“Ok tuachanane na hayo, vipi maandalizi yako ya kwenda kwenye hiyo mission?”

“Ndio kama hivi unavyo niona nazidi kujikaza, kwa maana nikicheza vibaya nakufa au nakamatwa na nisinge penda kukamatwa na wamarekani, ni bora nijipige risasi nife hapo hapo”

Maneno ya Agens yakamfanya Fetty kukaa kimya huku akimtazama Agnes usoni mwake, jinsi anavyo mwagikwa na jasho jingi.
 

  ***

Kila mmoja ndani ya maabara akaka kimya huku akimtazama Rahab, jinsi anavyo mchunguza mtu mmoja baada ya mwengine. Rahab akaachia tabasamu pana kisha akapiga hatua na kuingia ndani kabisa ya maabara huku nyuma yake akiingia mume wake pamoja na bosi wa bwana Frednando

“Jamani asanteni kwa ushirikiano wenu kwa kuweza kunihudumi hadi nimekuwa sawa”

Rahab alizungumza kwa furaha kubwa, ikamlazimu Frednando kuweza kuitafsiri kwa kispain. Madaktari walitabasamu kwa uwoga ila mioyoni mwao kila mmoja alikuwa akiliwazia lake kuhusiana na mbwa aliye fufuka dakika chache zilizo pita. Rahabu pasipo kuambiwa na mtu yoyote akaingia kwenye chumba alicho fungiwa mbwa huyo na kumchuku.

“Jamani mbwa huyu nimependa, anaitwa nani?”

Rahab akawauliza madaktari walio baki na mshangao mkubwa, kwa kingeraza ila mmoja wao akajikaza na kuzungumza kwa sauti ya utaraitibu.

“Anaitwa Charity”

“Waoo nitamchukua nimempenda sana”

Hakuana aliye kuwa na ubishi kuhusiana na kuchukuliwa kwa mbwa huyo, waliye mfanyia majaribio, ila kila daktari akabaki kimya. Hapakuwa na daktari aliye weza kuzungumza kwa kile walicho weza kukiona.

Wakarudi katika jumba la Frednando ambapo ikawalazimu kuwasiliana na ubalozi wa Tanzania uliopo nchini Mexco. Balozi baada ya kupokea simu ya raisi Praygod Makuya, ikamlazimu kuongozana na baadhi ya askari wa jeshi la Tanzania hadi kwenye jumba la Frednando, baada ya kufika wakapokelewa vizuri kama ilivyo kuwa kwa raisi wao.

“Yaani raisi siamini kama upo hai?”

Bi Joyce Maagi alizungumza huku akimtazama raisi Praygod machoni mwake.

“Nipo hai, nasikia nchini watu wapo kwenye maombolezo ya kifo change?”

“Ndio muheshimiwa hapa mwenyewe nilikuwa nimebakisha siku mbili niende kwenye msiba wako”

“ Ok ila sinto hitaji muweze kuzungumza kitu chochote kuhusiana na kuniona kwangu, nitahitaji kurudi siku ya mazishi yangu ninaamini nitakuwa Tanzania”

“Ila kikubwa ninacho hitaji wewe kukifanya nitengenezee mazingira katika uwanja wa ndege kwani nitakuja na private airplane(Ndege binafsi), wajulishe baadhi ya watu watakao nipokea kisiri mimi na mke wangu pasipo watu wengine kuweza kutambua lolote”

“Sawa muheshimiwa ila kuna swala la mke, si tayari amesha fariki au kuna mwengine”

“Yupo”

Raisi Praygod akamngong’oneza mmoja wa wahudumu Frednando na kumuagiza akamuite Rahab, naye akafanya hivyo. Baada ya muda Rahab akafika sebleni, akiwa amevalia gauni jeupe na refu lililo mpendeza sana. Bi Joyce Maagi akusita kumshangaa Rahab, kwani picha yake ipo kwenye moja ya watu wali angamia na ndege ya raisi.

“Huyu binti naye pia amepona?”

“Ndio amepona, ni mmoja wa watu walio weza kuyapigania maisha yangu hadi hapa nilipo”

“Ahaa”

Bi Joyce Maagi akanyanyuka na kwenda kusalimiana na mke wa rais, kwa heshima zote. Wakaendelea na mazungumzo ya kawaida. Siku iliyo fwatia Bi Joyce Maagi akaondoka akiwa na masafara wake kuelekea nchini Tanzania, kitu cha kwanza baada ya kutua katika uwanja wa mwalimu Jk Nyerere, akafanya maagizo yote aliyo agizwa na Raisi Praygod Makuya, japo baadhi ya watu walishangaa kusikia kwamba Raisi Praygod yu hai.

Maandalizi ya safari ya kurudi Tanzania, yakawekwa tayari na Frednando, akahakikisha kwamba kila kitu kipo salama na hakuna jambo baya ambalo litamdhuru raisi Praygod Makuya pamoja na mke wake. Ikawa ni siku nyingine ya huzuni kwa marafiki wawili Praygod na Frednando, kila mmoja Alisha mzoea mwenzake kwa kipindi kifupi walicho ishi, ila hapakuwa na jinsi yoyote yakufanya. Iliwalazimu kuweza kutengana tena na kila mmoja aweze kuendelea na majukumu yake anyo yafahamu.

“Shem siku une ikuli Tanzania”

Rahab alizungumza kwa furaha baada ya kuwaona Praygod na Frednando wakiwa wanalengwa lengwa na machozi ya uchungu

“Usijali Shem, nitakuja siku naamini nikija mutakuwa mumepata kijana mdogo”

“Hahaaa Mungu ni mwema, ombeni Mungu niwazalie kijana wa kiume ili aja kuwa raisi kama baba yake”

“Kwa nini usituzalie wa kike ili awe raisi labda wa kwanza, mwanamke kwa miaka hiyo ijayo?”

“Sawa Mungu ni mwema anaweza kutuwezesha katika hilo”

“Haya jamani niwatakie safari nje, ndege imesha washwa, hiyo mutaitumia katika matumizi yenu binafsi”