SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 12 Novemba 2016

T media news

Rio Ferdinand asema Cristiano ni mkali zaidi ya Ronaldinho


Mchezaji wa zamani ambaye sasa hivi amekua ndugu mchambuzi wa michezo amekua aki make headline na maneno yake mengi sana hasa akiwa anazungumzia mastaa wenzake wa soka.

Rio akiwa kwenye mahojiano na gazeti la Marca alifunguka na kusema kwamba alijua kwamba Ronaldo atakuja kuwa mkali zaidi ya Ronaldinho kama ilivyo sasa. Ferdinand anasema kwamba miaka 18 iliyopita alimwambia Sir Alex Ferguson kuhusu Ronaldo baada ya kucheza nae kwenye mechi ya kirafiki.

Rio anasema,“Nilimwambia Sir Alex kwamba tumsaini huyu kijana, tumemkosa Ronaldinho na kila mtu hajafurahia hilo. Lakini huyu ni mchezaji ambaye atakuja kuwa bora zaidi ya Ronaldinho”.

Rio anasema alimwambia maneno haya kocha Fergie mara baada ya mechi yao ya pre season ambayo Ronaldo alionyesha kiwango kizuri. Unadhani Ronaldo anaonyesha uwezo zaidi ya Ronaldinho.