SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 15 Novemba 2016

T media news

Orodha ya vyuo 26 vilivyofutiwa usajili na NACTE leo


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifungia vyuo vya ufundi 26 kutokana na makosa mbalimbali, ikiwamo kushindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa katika cheti cha usajili wa vyuo hivyo, huku likisimamsisha utoaji wa programu zilizokuwa zikitolewa katika vyuo 20 ambazo hazijasajiliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Kaimu Katibu mtendaji wa NACTE, Dkt. Adolf Rutayuga, alisema kuwa wamekuwa wakifuatilia vyuo vya ufundi ili kutathmini kama vinafuata viwango vya ubora wa kitaaluma vilivyowekwa na NACTE katika kutoa mafunzo.

 

Katibu huyo amesema kuwa baada ya kufanya uchunguzi huo, wamebaini vyuo 26 vilishindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na NACTE katika cheti cha usajili, huku vyuo 20 vikitoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa chini ya idara isiyotambulika,wakati vyuo viwili vikiwa na vituo vya satellite/Kampasi ambavyo navyo havijathibitishwa na chombo husika.

NACTE ni bodi iliyoanzishwa kisheria chini ya Sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, kifungu cha 129, kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo nchini Tanzania.  Chini ya sheria hiyo, ili kufikia na kudumisha hali ya mtoa mafunzo, vyuo vyote vinatakiwa viwe vimesajiliwa, vibali na kuwa mitaala iliyopitishwa na baraza. Vyuo haviruhusiwi kuanza kutoa kuanza kutoa huduma yoyote ya mafunzo bila idhini ya baraza.

 

Hapa chini ni mgwanyo wa vyuo katika makundi matatu na hatua zilizochokuliwa dhidi ya kila kundi

 

Jedwali 1: Vyuo vya Ufundi vilivyofutiwa usajili

S/NCHUO1Institute of Management and Development Studies – Iringa2Green Hill Institute – Mbeya3Institute of Business and Social Studies – Mbeya4Loyal College of Africa – Mbeya5Mbeya Training College – Mbeya6Mbengwenya College of Business and Information Technology –Mbinga7New Focus College – Mbeya8Shukrani International College of Business and Administration –  Mbeya9Majority Teachers College – Mbeya10Rukwa College of Health Sciences – Sumbawanga11MAM Institute of Education – Mbeya12Belvedere Business and Technology College – Mwanza13Geita Medical Laboratory Sciences and Nursing Training College – Geita14Global Community College – Geita15Muleba Academy Institute – Muleba16St. Bernard Health Training Institute – Katoro, Geita17Victoria Institute of Tourism and Hotel Management – Mwanza18Gisan Institute of Health Sciences – Mwanza19Dar es Salaam Institute of Business Management – Dar es Salaam20SAMFELIS College of Business Studies – Dar es Salaam21Ellys Institute of Technology – Bunda, Mara22Tanzania Institute of Chartered Secretaries and Administrators – Arusha23Emmanuel Community College – Kibaha24Modern Commercial Institute – Dar es Salaam25Marian College of Law – Dar es Salaam

Jedwali 2: Vyuo vya Ufundi vinavyotoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa

S/NCHUOMAFUNZO1MISO Teachers College – MafingaCompetence Building Network (CBN) – a Certificate in Early Childhood Education2Tusaale Teachers College – MafingaCompetence Building Network (CBN) – a Certificate in Early Childhood Education3The St. Joseph’s College Institute of Business and Management (SJCIBM) – Morogoro4The Golden Training Institute – Dar es Salaam5Nkrumah Mkoka Teachers College – Kongwa, Dodoma6National Institute of Agriculture (Chuo cha Kilimo cha Taifa) – Arusha7Musoma Utalii Training College – Musoma8Mwanza Polytechnic Institute – Mwanza9Mwanza Polytechnic Institute – Maswa10Ruter Institute of Financial Management – Mwanza11Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Mwanza12Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Geita13Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Bukoba14Singni International Training Institute – Bukoba15Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Kahama16Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Simiyu17Richrise Teachers College – Geita18Twiga Training Institute – Musoma19Zoom Polytechnic Institute – Bukoba20St. Thomas Training College – Shinyanga

Jedwali 3: Vyuo vya Ufundi vyenye Vituo vya Satellite / Kampasi

S/NCHUO1MISO Teachers College – Mafinga2Rungemba Teachers College – Mafinga