Kesi ya kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, inayomkabili Mbunge Jimbo la Arusha Mjini, Godbless lema na mke wake Neema Lema (33), imeshindwa kusikilizwa maelezo ya awali.
Hatua hiyo ni baada ya Mbunge huyo kukwama kuletwa Mahakamani toka Mahabusu kwa sababu zisizojulikana.
Kukosekana kwa Mbunge huyo kuonekana Mahakamani, kulimlazimu Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha Agustino Rwezile kutoa amri ya kutolewa hati ya kumtoa Mahabusu mshitakiwa huyo na kumleta mahakamani hapo ili kesi hiyo isikilizwe maelezo ya awali.
Hata hivyo tangu amri hiyo itolewe saa nne asubuhi hadi saa saba mchana mshitakiwa hakuweza kuletwa mahakamani hapo, licha ya mke wake kuwepo mahakamani hapo.
Rwezile alimtaka wakili wa serikali kueleza sababu za kushindwa kumleta Lema Mahakamani wakati Mahakama imetoa amri.
Wakili wa serikali Fotunatus Mhalila alisema mshitakiwa ameshindwa kuletwa Mahakamani kutokana na sababu zisizozuilika , ila kwa sababu upelelezi umekamilika aliomba Mahakama ipange tarehe ya usikilizaji wa hoja za awali.
Majibu hayo yalipingwa vikali na Wakili wa utetezi, John Mallya ambaye alitaka ufahamu sababu za kutomleta Lema anazodai hazikuweza kuzuilika ni zipi vema zikatajwa mahakamani. “Mheshimiwa hakimu hizo sababu zisizoweza kuzuilika ni zipi Wakili wa seriali atueleze, tujue kama siyo amedharau mahakama licha ya kutakiwa kumleta mshitakiwa,” alisema.
Baada ya hoja hizo utolewa Hakimu Rwezile aliendelea kusisitiza hati ya kumtoa Mahabusu itolewe ili aletwe Mahakamani leo katika kesi hiyo, ambayo itasikilizwa hoja za awali.
Awali katika kesi hiyo Godbless Lema na mke wake Neema, alisomewa mahitaka kuwa kati ya Agosti 20 Mwaka huu ndani ya Arusha,walimtumia ujumbe wa simu ya kiganjani Mkuu huyo wenye lugha ya matusi Mkuu huyo, huku wakijua ni kosa kisheria. Ilidaiwa kuwa ujumbe huo ulituma kutoka 0764150747 namba 0756551918 kwenda namba 0766-757575 uliokuwa ukidai, “Karibu, tutakuthibiti kama Uarabuni wanavyothibiti mashoga.” Washitakiwa walikana shitaka hilo na walipatiwa dhamana hadi leo itakaposomwa leo. huo.
Wakati huo huo, Waandishi wa habari walijikuta wakipata wakati mgumu kufanya majukumu yao, kutokana na askari wa Jeshi la Polisi wakishilikiana na askari wa Magereza walizuia kuingia chumba cha Mahakama na kufukunza nje ya fensi ya Mahakama kwa madai kuwa ni maagizo ya Mahakama.
Hata hivyo waandishi walilazimika kuandamana hadi kwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Agustino Rwezile, ambaye alikana Mahakama kutoa amri yoyote ya kuzuia waandishi kufanya kazi yao.
“Nawaomba msamaha na poleni kwa usumbufu mliopata, ila nitaongea na askari wa pande zote mbili ili tueleweshane, maana mnatekeleza majukumu yenu ya kikazi na kama barua tunawapatia za utambulisho na vitambulisho mnavyo kwa nini mzuiliwe hapo kuna tatizo tutaongea nao,”alisema