MTV Base ni moja kati ya vituo vya televisheni nguli na vyenye heshima zaidi Duniani, imekuwa na matawi kadhaa kila Pembe ya Mabara.Sio rahisi kutaja list ya Vituo 10 bora vya Televisheni kwenye upande wa Entertainment duniani ukaiacha MTV ambayo ina matawi sehemu nyingi duniani ikiwepo Afrika Kusini ambako kuna tawi liitwalo MTVBaseSA.
Sasa Luninga ya MTV Base south Africa, imetaja list ya marapa 10 wakali waliotisha zaidi kwa mwaka 2016. List hii kwa mujibu wa MTVBaseSA imepangwa kwa kutumia vigezo sita muhimu ambavyo ni..
Mapokeo na Matokeo ya nyimbo zao
Mtindo wa kuflow
Uandishi wa Mistari
Mauzo kwenye Muziki na Shows
Kujiamini
Kutobabaika wakati wa kuchana
Namba moja wamempatia rapa Fareed ‘Fid q’ Kubanda kutokea Mkoani Mwanza, Itazame list nzima hapo chini then tuachie maoni yako,