SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 14 Novemba 2016

T media news

Mane Aeleza El Hadji Diouf Kuwa Shujaa Wake, Ataka Kushinda Tuzo Ya Afrika Kama Yeye

 Mshambuliaji nyota wa Liverpool, Sadio Mane amesema angependa kushinda tuzo ya mwanasoka bora Afrika kama ilivyo kwa shujaa wake.

Shujaa wake ni mshambuliaji mwingine wa zamani wa Liverpool, El Hadji Diouf.

El Hadji Diouf ambaye alijulikana kwa soka safi lakini utukutu pia, aliwahi kuitumikia Liverpool ingawa hakudumu sana.

Mane sasa ni tegemeo la Liverpool katika upachikaji mabao na kuisaidia timu kushinda.