SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 13 Novemba 2016

T media news

DONALD TRUMP ASEMA HAITAJI HATA DOLA MOJSA KWENYE MSHAHARA WAKE AKIINGIA IKULU


“Sitachukua hata Dola moja kwenye mshahara wa Urais”, ni kauli ya Rais mteule Donald Trump baada ya kuulizwa kwamba atakuwa akiufanyia nini mshahara wa Dola laki nne (400,000 kwa mwaka) ambazo ni mshahara wa Rais wa Marekani anapokuwa Ikulu ya White House.

Kauli hii aliitoa Donald Trump mshindi wa kiti cha Urais nchini Marekani wakati akiwa kwenye kampeni zake September 17, 2015, huko Rochester, New Hampshire: “Kitu cha kwanza ninachotaka kuwaambia na nitakifanya kama nikichaguliwa kuwa Rais, Sitakuwa nikichukua mshahara, hata dola moja siihitaji, hicho sio kitu kikubwa kwangu.” – Donald Trump

Kwa mujibu ripoti mpya zilizotolewa na jarida la watu maarufu duniani Forbes, limetaja utajiri wa Rais huyo mteule kuwa unafikia Dola Bilioni 3.7 za Marekani ambazo ni zaidi ya shilingi Trilioni 8 za Tanzania

Katika Video hapa chini, Donald Trump anasikika akisema kwamba alikuwa akijigharamia kwa fedha yake mwenyewe wakati wa kampeni zake, hivyo hatachukua mshahara wake zaidi ya kupokea vitu vidogo ambavyo ni vya lazima akiwa Rais.