Brazil wametoa kipigo kikali dhidi ya mahasimu wao Argentina kwa kuwafunga mabao 3-0 kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Russia uliofanyika Uwanja wa Mineirão uliopo Belo Horizonte.
Uwanja huo una kumbukumbu mbaya kwa Brazil kufuatia kuwahi kupoteza kwa kipigo kizito cha mabao 7-1 kutoka kwa Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014.
Lakini safari hii hali ilikuwa tofauti kidogo baada ya kushuhudia wakishusha kipigo hicho kizito mbele ya mahasimu wao hao wa soka la Amerika ya Kusini.
Katika pambano hilo maarufu kama Superclássico das Américas magoli ya Brazil yamefungwa na Philippe Coutinho ambaye alifunga la kwanza kwa shuti kali la mbali baada ya kuwahadaa mabeki wa Argentina, la pili likwekwa kambani na Neymar na baadaye nyota wa zamani wa Tottenham Paulinho kuhitimisha karamu hiyo ya mabao.
Dondoo muhimu
Huu ni ushindi wa tano kwa kocha wa Brazil Tite tangu aichukue timu hiyo kutoka kwa mtangulizi wake Carlos Caetano Bledorn Verri maarufu kama Dunga mapema mwaka huu.
Brazil wanashika usukani kwenye mbio za kufuzu fainali za Kombe la Dunia kwa Amerika ya Kusini.
Argentina wameshindwa kupata ushindi katika michezo minne mpaka sasa, na wapo katika nafasi isiyoruhusu kufuzu.
Argentina wanashika nafasi ya sita kwenye msimao wa kundi.
Qualifying Tournament
#TeamPlGDPts1Brazil1117242Uruguay1115233Colombia113184Ecuador113175Chile112176Argentina11-1167Paraguay11-5158Peru110149Venezuela11-12510Bolivia11-224