SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 9 Oktoba 2016

T media news

WASTANI WA KIASI CHA FEDHA AMBACHO DIAMOND PLATINUMS HUINGIZA KWA SIKU


Maneno mengi sana yamesemwa kuhusu kiasi cha fedha analichonacho Naseeb Abdul a.k.a Diamondo Platnumz na vile vile unaweza kumuita Chibu Dangote au Baba Tiffah, na wengine kufikia hatua ya kusema anaweza kuwa ndiye msanii tajiri Afrika Mashariki kwa sasa.
Inasemekana kwamba, kwa kuangalia yote anayoyafanya msanii huyo unaweza kuwa na mwanga kiasi fulani wa kujua anaingiza kiasi gani.
Diamond Platnumz, kwa siku anaingiza wastani wa Sh. milioni 20 kutokana na kupakuliwa kwa nyimbo zake zilizoko kwenye mitandao: Kumbuka hii ni pembeni kabisa na shows anazofanya au malipo anayopokea kutoka kwenye makapuni anayoyafanyia matangazo kama Vodacom, Red Gold na NMB.
Na mpaka hapo utaamini sasa ule usemi wake wa siku zote kwamba muziki ni biashara! Na wasanii wengine hawana budi kumuiga Diamond Platnumz, wawe na wivu wa maendeleo na sio kutamani kumshusha alipo sasa.