SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 18 Oktoba 2016

T media news

Wajeruhiwa kwa bomu wakimkamata mtuhumiwa

Kigoma. Polisi na raia wanne wamejeruhiwa kwa bomu la kutupwa kwa mkono walipokuwa wakimkamata mtuhumiwa wa ujambazi kwenye Kijiji cha Uvinza mkoani Kigoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 14.

Mtui aliwataja majeruhi hao kuwa ni askari polisi F.3187 Koplo Isaya na raia Saidi Mohamed, Seleman Kashali, Joseph Daudi na Hassan Nasibu, wote wakazi wa Kijiji cha Uvinza.