Klabu ya Yanga inapenda kuwatangaazia wanachama wote wa Young Africans Sports Club (Yanga) kuwa patakuwa na mkutano mkuu wa dharura siku ya Jumapili ya tarehe 23/10/2016.
Wanachama wote mnaombwa kufika bila kukosa ikiwa ni kwa faida na maslahi mapana ya timu yetu.
Agenda za mkutano pamoja na mahali mkutano mkuu utakapofanyika mtajulishwa mapema kabla ya siku husika kufika.
‘YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO’
Imetolewa na uongozi – Young African Sports Club.