SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 18 Oktoba 2016

T media news

NICKI MINAJ AMPONDEA DONALD TRUMP NA MKE WAKE KWENYE TAMASHA LA TIDAL X

Mastaa wa Marekani wameendelea kumuandama mgombea wa Urais wa Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump – sasa ni zamu ya Nicki Minaj.

Kwenye tamasha la Tidal X 1015 lililofanyika wikiendi hii huko mjini New York, rapper Nicki Minaj alimponda mgombea huyo anayechukiwa na watu wengi kwa vitendo vyake vya udhalilishaji kwa wanawake pamoja na sera zake za kuwapinga watu weusi.

“Barack needed Michelle, bitch, and Bill needed a motherf-cking Hillary. You better pray to God you don’t get stuck with a motherf-cking Melania,” amesema Nicki wakati wa tamasha hilo.

Mpaka sasa mastaa kadhaa wameonekana kumpinga mgombea huyo akiwemo Jon Stewart, Barbra Streisand, Samuel L. Jackson, Chelsea Handler, Lena Dunham na wengine.