Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameeleza mipango ya kuondoa sheria ambayo inalalamikiwa na wengi kwa kushindwa kutoa nafasi kwa wawekezaji wa nje.
Sheria hiyo inayataka makampuni mbalimbali ya kimataifa kutoa hisa nyingi kwa raia wa Zimbabwe.
Kwa sasa sheria hiyo haina nguvu sana na Rais Mugabe anataka kuona uchumi wa nchi hiyo ukiimarika.
Sheria hiyo inalalamikiwa vikali na mashirika ya fedha ulimwenguni IMF kwa kusababisha kuanguka kwa uchumi wa Zimbabwe.
Kumekuwa na maandamano dhidi ya serikali katika miezi ya hivi karibuni, kutokana na kudorora kwa uchumi wa taifa hilo la Kusini mwa Afrika.