SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 11 Oktoba 2016

T media news

Msimamo wa TFF kuhusu Yanga kukodishwa kwa kampuni ya Yanga Yetu Limited

Siku chache baada ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kutangaza kutotambua mabadiliko ya klabu ya Yanga kukodishwa na kampuni ya Yanga Yetu Limited, leo October 11 shirikisho la soka nchini TFF limetangaza msimamo wake juu ya mabadilko yaliyofanywa na klabu hiyo.

Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa amesema, TFF inatambua hadi sasahivi Yanga bado ipo kama ilivyokuwa zamani, mabadiliko yaliyofanywa yatatambuliwa hadi pale watakapokuwa wamesikia kutoka kwa Yanga wenyewe.

“Hadi sasa, Yanga bado ipo kama ilivyokuwa zamani chini ya taratibu za TFF, CAF na FIFA. Mabadiliko mengine zaidi ni baada ya kuwa tumesikia kutoka kwao wenyewe,” amesema Mwesigwa mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa msimamo wa TFF kuhusu Yanga kukodishwa.

“Kwa maana nyingine, kwa wale wanachama waliokuwa wanakuja kwangu wanasema wanataka kumuona mkuu wa nchi, sisi tunawaambia kwamba klabu ya Yanga tunavyoitambua ipo chini ya Mwenyekiti wake na Katibu wake, utaratibu uliopo ni uleule uliokuwepo tangu zamani.”

Yanga walishatoa mkataba wa timu yao kukodishwa na kampuni ya Yanga Yetu Limited lakini tangu mkataba huo kuwekwa hadharani bado mamlaka zinazosimamia michezo nchini zimesema hazitambui mabadiliko yoyote yaliyofanywa na klabu hiyo.