Bayer Liverkusen ilikuwa mwenyeji wa Spurs kwenye game ya Champions League usiku wa October 18 mchezo uliovihusisha vilabu vya Ujerumani na England.
Spurs bado wanamwendo wa kusuasua kwenye michuano hiyo ya Ulaya na walikuwa wanataka kuhakikisha hawapotezi mchezo huo kwa gharama yeyote katika usiku wa jana.
Shukurani za pekee zinakwenda kwa golikipa wa Spurs Hugo Lloris aliyeisaidia timu yake kupata pointi moja ya ugenini.
Golikipa huyo mfaransa aliokoa mpira kwenye mtari wa goli wakati ukielekea nyavuni na kufanya matokeo kuwa 0-0 hadi mwisho wa mchezo.
Star wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez ‘Chicharito’ alikuwa na uhakika kuiandika Liverkusen bao la kuongoza, lakini goal-line technology ilionesha Lloris alifanya kazi ya ziada kuliweka lango lake salama.