Wiki hii historia mpya imewekwa nchini Italy baada ya mshambuliaji
wa Vicenza inayoshiriki Ligi ya Serie B, Cristian Galano kuzawadiwa kadi ya kijani kwa kucheza mchezo wa kiungwana (fair play). Maafisa wa soka nchini Italy mwanzoni mwa msimu huu walitangaza matumizi ya kadi hiyo na kusema mchezaji atayekuwa na kadi nyingi zaidi za kijani atapewa zawadi mwishoni mwa msimu.
Kadi hiyo ilitolewa baada ya Galano kukiri kwa mwamuzi kuwa, hakukuwa na beki yeyote wa Virtus Entella aliyegusa mpira ambao mwamuzi Marco Mainardi aliamuru kupigwa kona.
Rais wa Serie B Andrea Abodi amekiri kwamba kadi hiyo ipo kama alama tu, lakini yenye mantiki ya kuifanya ligi hiyo kuwa na mtazamo chanya kufuatia kukabiliwa na tuhuma mbalimbali za upangaji matokeo.
“Ni kadi ambayo ipo kama alama tu,” amesema “Ni kitu rahisi tu. jambo muhimu hapa ni kujua tu kwamba mtu hupewa pindi anapofanya jambo la kiweledi zaidi. “Sisi tunaamini kwamba mchezo wa soka unahitaji ujumbe weye kuijenga jamii yenye mtazamo chanya,” Ofisa Habari wa Serie B aliongeza.“Kumbuka mchezo huu wakati mwingine unaweza kusababisha hasira kwa watu mpaka wakatoka uwanjani