SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 13 Oktoba 2016

T media news

Governor wa Mombasa Kumleta Nicki Minaj Baada ya Chris Brown

Inavyoonekana kaunti 001, au ukipenda kaunti ya Mombasa inatarajiwa kupata masupastaa mpwito mpwito mwaka huu.

Baada ya kumleta Chris Brown Mombasa, Gavana wa Mombasa, Gavana 001, almaarufu Sultan au ukipenda Ali Hassan Joho aliwapa ahadi mashabiki waliohudhuria tamasha la #MombasaRocks, kuwa atamleta Nicki Minaj kuperform Mombasa.

Chini ya ministry ya Tourism, kaunti ya Mombasa imekuwa mstari wa mbele kukuza jina lake kupitia matamasha mbalimbali yanayoandaliwa ili kuipa sifa kaunti hii kwenye sekta ya Utalii.
Hivyo basi, wapenzi wa Nicki Minaj kaeni tayari.