SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 13 Oktoba 2016

T media news

Barcelona kukutana na Real Madrid

Image captionMechi ya El Classico kati ya Real Madrid dhidi ya Barcelona

Mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uhiispania La liga uliobadilishwa jina na kuwa El Clasico ambao huzikutanisha timu hasimu Barcelona na Real Madrid umepangwa kufanyika Disemba 3 mwaka huu ambapo Barcelona watakuwa nyumbani.

Msimu uliopita Madrid ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 katika uwanja wa Camp Nou lakini nao walijikuta wakitandikwa mabao 4-0 katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Atletico kwa sasa ndio wanaongoza La Liga wakifuatiwa na Madrid katika nafasi ya pili na Barcelona wao wanashika nafasi ya nne.

Mchezo huo utafanya mashabiki wa soka wa Uingereza wakishindwa kuona mechi ya moja kwa moja katika runinga kutokana na muda uliopangwa.

Sheria za Uingereza zinakataza mechi kuonyeshwa moja kwa moja katika runinga nyakati fulani ili kuhamasisha watu wengi waende viwanjani kushuhudia timu zao zikicheza.

Wakati huo huo mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi amerejea rasmi mazoezini na klabu hiyo baada ya kupata majeruhi ya nyonga.

Nyota huyo alipata majeruhi hayo mwezi uliopita katika mchezo dhidi ya Atletico Madrid uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Barcelona ilithibitisha nyota huyo kurejea mazoezini katika kituo chao cha Ciutat Esportiva, ingawa walishindwa kueleza kama atakuwa fiti kwa ajili ya mechi za mashindano.

Barcelona inatarajiwa kukutana na Deportivo La Coruna Jumamosi huku beki wake Samuel Umtiti naye akirejea mazoezini kufuatia kupona jeraha la goti.