Nyota wa Barcelona Lionel Messi amefichua sababu zilizomfanya abadilishe mwonekano wa nywele zake kuwa nyeupe.
Nahodha huyo wa Argentina aliushangaza ulimwengu kutokana na kuamua kuja na mwonekano huo ambao watu hawakudhani kama angekuja kufanya vile.
Alipoulizwa sababu za kuamua kufanya vile, Messi alijibu kwamba ilikuwa ni sehemu ya kujfariji baada ya nchi yake ya Argentina kushindwa kutwaa ndoo ya Copa America.
“Ilikuwa ni siku ngumu sana kuwahi kutokea katika maisha yangu hasa ya soka, ndiyo maana nilifanya vile nikiamini kwamba natakiwa nianze kila kitu upya,” alisema wakati akihojiwa na mchekeshaji Kiargentina Mingo kwenye kwenye programu ya comedy ya Telefe’s ‘Polemica en el bar’.
Messi alienda mbali zaidi na kusema hadhani kama mwanawe wa kwanza Thiago anafuata nyayo zake kutokana na kutoonesha kuvutiwa na mchezo huo kipenzi cha wengi.
“Kwa sasa najaribu kutompa Thiago mpira achezee kwasababu haoneshi kuupenda mchezo huo,”
“Tutaona kama baadaye ataanza kuvutiwa kwasababu sasa hivi ameanza kucheza na watoto wenziwe klabuni.”