Alexander Kinyua (kushoto) na mwanamume aliyekuwa akiishi naye nyumba moja Kujoe Bonsafo Agyei-Kodie. Picha/MAKTABA
Mwanafunzi kutoka Kenya aliyekuwa akiishi Marekani amekiri kwamba alimuua mwanamume waliyekuwa wakiishi nyumba moja na kula moyo wake na ubongo wake.
MWANAFUNZI kutoka Kenya aliyekuwa akiishi Marekani amekiri kwamba alimuua mwanamume waliyekuwa wakiishi nyumba moja na kula moyo wake na ubongo wake.
Alexander Kinyua, 22, alikiri mashtaka ya mauaji ya Kujoe Bonsafo Agyei-Kodie, 37, katika jimbo la Maryland mwaka jana lakini Jaji akasema hafai kulaumiwa aliposhtakiwa Jumatatu wiki hii.
Jaji Stephen Waldron alisema Kinyua hawezi kulaumiwa kwani alikuwa anaugua akili na akaagiza awekwe kwenye hospitali ya watu wenye akili punguani.
Kinyua, aliyekuwa mwanafunzi wa uhadhisi katika chuo cha Morgan State, aliambia maafisa kwamba alitumia kisu kuua mwenzake kabla ya kula viungo vyake.
Agyei-Kodie, mzaliwa wa Ghana, aliishi na Kinyua nyumba moja kwa wiki sita kabla ya kutoweka kwake Mei 2012.
Kinyua awali alikana kujua kuhusu kifuo cha mwenzake, lakini mwishowe akawapeleka maafisa hadi jaa la kanisa ambapo alikuwa ameficha mwili wa marehemu.
Dawa
Mauaji hayo yalitokea Kinyua akiwa nje kwa dhamana kwa kumshambulia kwa mkwaju wa kucheza besiboli mwanafunzi mwenzake wa zamani.
Kinyua alimwacha Joshua Ceasar mnamo Mei 19, 2012 akiwa karibu kipofu baada ya kumshambulia.
Mahakamani Jumatatu Kinyua alijibu maswali ya jaji kwa upole na alisema dawa ambazo amekuwa akipewa zimekuwa zikimsaidia.
Uchunguzi wa hali yake ya kiakili ulibaini kuwa alikuwa anaugua ugonjwa ambao wa Kiingereza hujulikana kama ‘paranoid schizophrenia