SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 26 Agosti 2016

T media news

Warioba ajibu hoja ya Kingunge kuhusu Magufuli

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Kingunge Ngombale-Mwiru aliwataka Marais wastaafu na Mawaziri Wakuu wastaafu nchini kuingilia mvutano wa kisiasa unaoendelea sasa kuhusu Ukuta kutafuta muafaka kwa Rais Magufuli.

Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba  alisema viongozi wakuu wastaafu ambao ni marais na mawaziri wakuu wamekuwa wakimshauri Rais katika masuala mbalimbali.

“Kweli tuko kimya lakini ukimya huo usitafsiriwe kuwa hatumshauri Rais sisi kama viongozi wastaafu, lakini haifanyiki kwenye vyombo vya habari,” alisema Jaji Warioba.

Jaji Warioba alisema badala ya kumjibu Kingunge ni vyema kumuachia Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi awakutanishe viongozi wa vyama vya siasa kujadili hali hiyo kwa lengo la kupata muafaka.

Hata hivyo, alisema ni wajibu wa Watanzania wote kuhakikisha wanalinda hali ya amani nchini badala ya kuliona jambo hilo linamhusu Rais John Magufuli pekee au mtu mwingine yeyote. “Tumsaidie msajili katika hili, hili sio tatizo la mtu mmoja bali ni la nchi nzima tusimuachie Rais,” alisema Jaji Warioba.