SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 4 Agosti 2016

T media news

Taribo West: Hivi ndivyo Nigeria tulivyoweka historia Olimpiki 96


 Mnamo 3 August 1996, Nigeria ilitengeneza historia ya kuwa nchi ya kwanza ya kiafrika kuwa mabingwa wa Olympic iliyofanyika Atlanta nchini Marekani.  

Kwa Taribo West, mchezaji wa zamani wa vilabu vya Auxerre, AC Milan na Inter Milan,  ushindi wa 3-2 dhidi ya Argentina katika fainali bado upo kwenye kumbukumbu zake kila siku.   

” Olympics ya 1996 ni moja matukio makubwa kwenye maisha yangu.  Tulikuwa na kikosi ambacho kingeweza kupambana na yoyote duniani. ” 

West anasema michezo ya kujiweka sawa kuelekea mashindano,  chini ya uongozi wa kocha wa kidachi Jo Bonfrere,  ziliwasaidia pamoja na kufungwa na Togo, katika mchezo wa mwisho wa kirafiki wa mwisho kabla ya kuelekea USA.  

“Kabla ya Olympics, tulikuwa tumejiandaa vizuri. Tulipofika USA hatukupumbazwa na vitu vigeni kwetu.  Tulikuwa makini na mtihani uliokuwa mbele yetu.  Maandalizi ya timu ya kocha Jo Bonfrere yalikuwa mazuri sana.” 

Baada ya mechi ya kwanza ya ufunguzi ya ushindi wa 1-0 vs Hungary,  kisha ushindi wa 2-0 dhidi ya Japan, Super Eagles wakapoteza 1-0 dhidi ya Brazil katika mchezo wa mwisho wa kundi D mjini Orlando, Florida.  

 

Baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Mexico katika mchezo wa robo fainali, the “Dream Team”, kama walivyoiita wanaija wenyewe wakapangwa kucheza na Brazil kwa mara nyingine tena,  safari hii kwenye nusu fainali, moja ya mechi kali za michuano hiyo.  

Baada ya kutanguliwa kwa 3-1 katika kipindi cha Kwanza,  wanaigeria wakawa na mlima wa kupanda. 

“Tulijua kwamba kipindi cha kwanza cha mchezo tulicheza vibaya sana,  lakini kilichopelekea kurudi kwetu  mchezoni katika kipindi cha pili kulitokana na hitaji letu la kutaka kushinda. 

“Sauti za viongozi zilisikika kwenye chumba cha kubadilishia nguo.  Tulishinda ile mechi ndani ya dressing room.

“Kwa bahati nzuri,  tulikuwa na wachezaji kama Daniel Amokachi, Sunday Oliseh na Uche Okechukwu. Ilikuwa jambo kwetu.”

Victor Ikpeba, mshambuliaji wa AS Monaco ambaye alishinda tuzo ya mchezaji bor wa Africa mwaka huo baadae, aliifungia Nigeria goli la pili dakika ya 78 ya mchezo.  

Lakini wakati Jay-Jay Okocha alipopoteza nafasi ya kusawazisha,  akikosa penati huku zikiwa zimebaki dakika chache kabla ya mchezo kuisha,  mechi ilionekana imemalizika.  

Hisia hizo ya kushindwa hazikuwemo kichwani mwa Nwankwo Kanu, ambaye aliweka kambani goli la kusawazisha dakika ya 90 ya mchezo kabla ya kuongeza goli la ushindi dakika 4 ndani ya extra time. 

Baada ya ushindi wa kushangaza dhidi ya timu iliyokuwa ikiundwa na wachezaji kama Bebeto, Roberto Carlos na Ronaldo, ambao walikuwa wametoka kushinda ubingwa wa dunia miaka 2 nyuma,  West anasema Wanaigeria walikuwa na uhakika wamepata nafasi ya dhahabu katika fainali dhidi ya Argentina,  katika uwanja wa Sanford huko Athens, Georgia.

“Kulikuwa na kitu mioyoni yetu kilichotupa imani kwamba tunaenda kushinda,  ingawa hatukujua tungeshindaje.  

“Mara tu baada ya Argentina kufunga goli la kwanza,  hatukuvunjika moyo, tulipigana na Amunike akafunga goli la ushindi.  

“Wakati [ referee Pierluigi] Collina alipopuliza kipenga cha mwisho, nilidondoka chini na nikajua ndoto yangu imekuwa kweli. 

“Medali yangu ya dhahabu ipo katika bank nje ya nchi,  ni kitu ambacho nimekiifadhi kwa ajili nije kuwaonyesha watoto wangu. ”