SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 6 Agosti 2016

T media news

MWENYEKITI WA YANGA YUSUF MANJI ATANGAZA KUIKODISHA YANGA KWA MIAKA 10


Manji akizungumza kwenye mkutano huo.
Hali ilivyokuwa nje kabla ya wanachama kuingia ukumbini.


Wanachama wa Yanga wakiwa ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam wakisubiri kuanza kwa Mkutano huo wa dharura ulioitishwa na Mwenyekiti wao, Yusuf Manji.
  Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji akiwasili ukumbini.
Yusuf Manji akisalimiana na wanachama wa Yanga.
Mkutano ukianza.

MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji ametangaza kuikodi klabu hiyoi kwa miaka 10 wakati akifanya mkutano mkuu wa dharula na wanachama wa klabu hiyo uliofanyika leo Jumamosi Agosti 6 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee eneo la Upanga jijini Dar es Salaam.

Baada ya kusalimia  na wanachama wake, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameanza kuzungumza na wanachama wa klabu hiyo kwenye na kusema haungi mfumo wa hisa kwa kuwa ni klabu ya wanachama.

Maneno hayo ya Manji, maana amewashangaza wengi waliokuwa wakiamini kuwa leo anakwenda kuomba kuinunua Yanga baada ya Mohammed Dewji maarufu kama Mo kutoa pendekezo la kununua Simba kwa asilimia 51 akitoa bilioni 20.

Pamoja na hivyo, Manji ameweka msisitizo katika suala la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwamba limekosea kuipa Azam FC nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho wakati Yanga ndiyo mabingwa.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Manji amesema amesikia kuna mtu ametoa Sh milioni 100 kuisaidia klabu moja na kuonekana ni mtu mwema Tanzania nzima hali ambayo inamshangaza kwa kuwa kusaidia kwa upande wa Yanga tena kwa gharama ya juu ni jambo la kawaida kabisa.

Ingawa Manji hajataja jina, lakini mfanyabiashara Mohammed Dewji alitoa Sh milioni 100 kusaidia usajili wa Simba.

“Nasikia wanasema ndiye tajiri namba moja Tanzania, ametoa Sh milioni mia kuisaidia klabu,” alisema Manji na wanachama wakashangilia.

Manji amekata kiu ya kile ambacho wanachama wengi na wapenda soka nchini walikuwa wakikisubiri kwenye mkutano wa dharura aliouitisha.

Baada ya kujadili, wanachama wa Yanga pamoja na wajumbe wa bodi wakapitisha kumkodisha Manji kwa miaka kumi kama alivyoomba.

Katika mkutano huo unaofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam kipindi hiki, Manji amesema amepeleka ombi la kuikodisha Yanga kwa miaka 10.

“Nitaikodisha kwa asilimia 75 na 25 inabaki kwa wanachama. Nataka kuikodisha timu na nembo, majengo ya klabu yanabaki kuwa mali ya wanachama.

“Katika miaka 10, ikipatikana faida 25 inakwenda kwa wanachama na klabu na 75 kwangu. Kama itakuwa ni hasara basi inakuwa hasara yangu, hakuna hasara upande wa wanachama au klabu,” alisema.

“Tayari nimewasilisha ombi hilo Bodi ya Wadhamini ambao wao watazungumza na nyinyi wanachama na kama kutakuwa na makubaliano basi tutaingia mkataba,” alisema Manji.

Manji alisema masuala ya timu kuhusu usajili, mishahara, uendeshaji kama safari na gharama nyingine zitakuwa chini yake.

Pia asilimia 25 ambayo itakuwa ni ya klabu, ndiyo itatumika kuujenga Uwanja wa Kaunda na Yanga itakuwa na uwanja wa kufanyia mazoezi na ikiwezekana hata kuchezea mechi.

Wanachama wengi walionekana kufurahi na wengi walisisitiza kwamba wanakubali hata kabla ya kuanza kwa mchakato huo rasmi.