STAA MUIGIZAJI wa muda mrefu kwenye tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa wazo la kuolewa tena kwenye akili yake halipo badala yake anaangalia mambo mengine kwenye maisha yake.
Akizungumza Johari, alisema kuwa siku zote ngojangoja huumiza matumbo sasa ameshakata tamaa ya kumpata mwanaume wa kumuita mume hivyo anajipanga kurudi shule.
“Kiukweli mawazo ya kuolewa tena sina, nimeshajikatia zangu tamaa, bora niangalie ustaarabu mwingine ikiwemo kurudi shule,” alisema Johari.