• Inapunguza maambukizi ya wadudu waharibifu kwa kua nyumba hii huzungushiwa wavu maalum kwa ajili ya kuzuia wadudu kuingia ndani.
• Mavuno yanakuwa hata mara kumi hadi kumi au zaidi kuliko kilimo cha eneo la wazi,ikitegemewa sana na aina ya mazao yanayolimwa,aina ya greenhouse na vifaa vya kudhibiti mazingira ya ndani ya green house.
• Uhakika wa kuvuna mazao mengi na yenye ubora wa kimataifa unaongezeka.
• Uzalishaji wa mazao katika kipindi chote cha mwaka,maana hamna haja ya kusubiri mpaka msimu wa zao ufike ndio ulime.
• Matumizi ya maji ni madogo sana na udhibiti wake ni rahisi mno.Aina ya umwagiliaji unaotumika hapa ni umwagiliaji wa matone ambao umuwezesha mkulima kumwagilia mimea pekee na sio magugu.
Kumbuka:- Green house pekee sio uhakika wa asilimia zote kukupatia mazao mengi na bora, lazima uzingatie upandaji wa mbegu bora ambazo ni maalum kwa kilimo cha greenhouse. Pia uzingatie uwekaji mzuri wa mbolea, uthibiti wa magojwa na kumwagilia maji kwa wakati.