SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 25 Agosti 2016

T media news

Huyu ndiye mkenya aliye na kucha ndefu zaidi


Mkenya John Waweru anayetumia kucha zake kama kivutio cha utalii. PICHA/Larry Madowo

  Mkenya wa miaka 34, John Waweru, ananuia kuvunja rekodi ya dunia kwa kuwa mtu aliye na kucha ndefu zaidi. Tayari kucha zake zina urefu wa sentimita 30

–Rekodi hiyo imeshikiliwa na raia wa India Shridhar Chillal aliye na ndefu zaidi kwa mkono mmoja

Mkenya ananuia kuingia katika kitabu cha kumbukumbu za dunia kwa kuwa mtu aliye na kucha ndefu zaidi ulimwenguni.

John Waweru mwenye umri wa miaka 34 alisema kucha zake zilizo katika mkono wake wa kushoto ndio chumo lake la kipekee maishani.

 John Waweru. PICHA/Larry Madowo

“Hii ndio kazi yangu, hupata chakula kutokana na maonyesho ya kucha zangu kwa kuzuru maeneo ya watalii kama vile Pwani. Watalii hulipa kutazama kucha zangu,” alisema mwanamume katika mahojiano na Daily Nation, Mombasa.

Mkenya huyo hupata kati ya Sh2, 000 na Sh10, 000 kwa siku kutokana na maonyesho ya kucha hizo.

Shridhar Chillal kutoka India aliyevunja rekodi ya dunia ya mtu aliye na kucha ndefu zaidi ulimwenguni
Amejenga nyumba ya vyumba vinne Mombasa kutokana na mapato hayo.

Lakini hawezi kujifanyia chochote kama vile kupika au kufua nguo kutokana na urefu wa kucha hizo.