Ni Shangwe huku gari la Mkuu wa mkoa likisukumwa na wananchi wenye furaha kijiji cha Mpuguso baada ya Mkuu wa mkoa kupokea na kukabidhi msaada wa mifuko 150 ya saruji kutoka kiwanda cha saruji mbeya ikiwa ni maombi ya Mkuu wa Mkoa Amos Makalla kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kituo cha afya kata ya Mpuguso. Viongozi ngazi zote na wananchi wamemshukuru sana mkuu wa mkoa kwa upendo kwa wananchi wa kata ya mpuguso
Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa mkoa Amos Makalla alisema aliamua kuomba msaada huo wa saruji na siyo fedha ili achangie ujenzi wa kituo cha afya ili kuonyesha kwa vitendo kuridhia ujenzi wa kituo cha afya eneo jipya baada ya kusitisha ujenzi wa zahanati mwezi April mwaka huu ujenzi wa zahanati kwenye eneo lilikuwa na mgogoro " Ndugu zangu leo ni furaha nimeamini wagombanao ndiyo wapatanao mwezi April
nilisitisha ujenzi wa zahanati kule kwenye eneo la mgogoro nikapendekeza eneo hilo nafurahi leo hatujengi zahanati tunajenga kituo cha afya, kuna niliyowakwaza ila nilizingatia sheria na kanuni, nimeona mlivyoanza vizuri ujenzi, nawapongeza wote na niliomba nami nichangie nashukuru Mbeya cement walinikubalia ombi langu na leo wameleta mifuko 150 ya saruji sasa ni kazi tu nipo nanyi mpaka tukamilishe ujenzi"
Amewashukuru Mbeya cement kwa msaada huo na amewaomba wadau wengine kuchangia kwani ili kukamilisha ujenzi wa kituo hicho kunahitaji fedha sh milioni 495
Amewaomba wananchi kushiriki kikamilifu hatua kwa hatua na yeye kama mlezi anataka kufikia juni mwakani kituo hicho kikamilike