Mtunzi: Enea Faidy
...DORICE alikuwa akiyatafakari maneno ya malkia wa himaya aliyokuwepo kwa wakati ule. Alikuwa haelewi afanye nini na achague lipi kati ya kifo au kuolewa na jini. Alijikuta yupo kwenye wakati mgumu sana mpaka akajuta kutoroka shuleni. Alimlaani sana Doreen kwani ndiye chanzo cha matatizo yote. Alijikuta analia bila kujua msaada wake utatoka wapi.
Akiwa katika wimbi la mawazo alishtushwa na harufu Kali ya marashi iliyomfanya azinduke na kumtazama mgeni wake. Alipoinua kichwa chake alikutana tabasamu mwanana kutoka kwenye sura nzuri ya upole ya kijana Mansoor.
"Nakupenda Dorice.. Olewa na Mimi!" Alisema mansoor kwa sauti tamu iliyojaa huba. Lakini sauti na maneno hayo habvikuwa kitu kwa Dorice, aliachia sonyo Kali iliyodhihirisha chuki kuu dhidi ya Mansoor.
"Kama kuniua niueni! Siwezi kuolewa nawewe!" Dorice alisema maneno hayo kwa ujasiri sana bila kujali jambo hilo lingeonekanaje kwa Mansoor.
Mansoor alihuzunika sana, akatikisa kichwa kama ilivyokuwa kawaida yake . Akashindwa kuyazuia machozi ya damu machoni mwake lakini Dorice hakujali hilo.
"Dorice! Kwanini haunipendi? Au kwa sababu Mimi sio binadamu mwenzio?" Aliongea Mansoor kwa huzuni sana lakini Dorice hakujibu kitu.
"Tafadhali niambie Dorice... Nikufanyie nini ili uamini kuwa nakupenda?" Aliuliza mansoor kwa sauti ya upole.
"Utanifanyia?"
"Ndio Dorice!"
"Naomba unirudishe duniani..."
"Nikikurudisha sasa nitakuoaje? Siwezi ishi mbali nawewe!"
"Umesema utanifanyia nikuombacho.. Umeniahidi!"
"Ndio ila hilo suala gumu... Kwanini hunipendi?"
"Nampenda mtu mwingine.. Na ndie aliyenifanya nipate matatizo haya yote.." Dorice alisema maneno hayo huku machozi yakimlengalenga kwani kila alipomkumbuka Eddy alidondosha chozi na hakutaka kuamini kama Kweli Eddy amemwacha na yupo na Doreen.
"Unampenda nani?"
"Nampenda mtu anaitwa Eddy, siko tayari kimkosa nataka nipiganie penzi langu... Samahani sana Mansoor... Wewe ni mzuri ila sins hisia na wewe kabisa!" Dorice alijikuta akiropoka maneno hayo yote ili kufikisha hisia zake kwa Mansoor. Maneno Yale yaliugusa vyema moyo wa Mansoor, alihuzunika sana ila ilibidi akubaliane na ukweli.
"Nashukuru kwa kuwa mkweli Dorice.. Nakupenda sana ila siwezi kukulazimisha unipende... Hakutakuwa na mapenzi hapo.. . Naumia sana ila inabidi nizielewe hisia zako!" Alisema Mansoor kwa sauti iliyojaa masikitiko makubwa sana ila hakuwa na jinsi. Mansoor alikuwa ni mini mstaarabu kupita kiasi ingawa mama take alikuwa katili tena mwenye roho mbaya sana.
"Umenielewa Mansoor?!"
"Ndio.. Nimekuelewa sana! Ila nisimulie ilikuwaje?"
Dorice alifuta machozi na kutabasamu kidogo ingawa bado alikuwa na maumivu ya mapenzi kwa Eddy. Akajua ule ni msaada wa kwanza kwake kwenye eneo lile, akaamua kumsimulia kila kitu kama ilivyokuwa kati ya yeye na Eddy na kisa cha kutoroka.
Mansoor alihuzunika sana, akamwonea huruma sana Dorice.
"Binadamu wabaya sana..!"alisema Mansoor.
"Inaniuma sana! Nampenda sana Eddy..!"!
Mansoor alichukua kitu kama kioo, akakitazama kwa muda kisha kikamletea picha ya Doreen.
"Mh! Huyu Doreen.. Ni mtu mbaya sana .. In mtu hatari kupita kawaida..!"
Alisema Mansoor kwa mshtuko huku akimtazama Dorice. Dorice alikuwa haelewi chochote akabaki akishangaa tu.
"Doreen ni mchawi sana.. Na kuna kitu anatafuta! Amemharibu sana Eddy... Eddy yupo kwenye wakati mbaya na muda wowote anammaliza..!"
Maneno ya Mansoor yalimshtua Dorice
"Amemfanyaje? Nisaidie kumwokoa Eddy tafadhali..!"
"Mama hatanikubalia ila inabidi nikusaidie Dorice.. Yote ni kwasababu nakupenda.. Nitakusaidia usijali!"
Alisema Mansoor.
"Nitafurahi sana ukinisaidia Mansoor!"
"Usijali.. Ila mama ni kikwazo..!"
"Jitahidi Mansoor!"
Dorice alichanganyikiwa sana baada ya kusikia kuwa Eddy atauliwa muda wowote na Doreen, ilibidi azidi kumsihi Mansoor aweze kumsaidia kwa namna yoyote ile kwani alitambua uwezo mkubwa aliokuwa nao jini yule mstaarabu.