SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 6 Julai 2016

T media news

LRiwaya :Mwanafunzi Mchawi(A Wizard Student) - Sehemu ya Kumi.


MTUNZI: ENEA FAIDY

 Ilipoishia Sehemu ya 9

......Ghafla wanafunzi wenzake wakabaki kumshangaa Eddy, wakaanza kukonyezana kisha wote wakaanza kumtazama Eddy kwa wizi.

Eddy hakujua lolote akaendelea kuoga kwa kujiachia sana.

Wanafunzi hao wambeya hawakukomea hapo Bali walitoka nje na kuwaita wenzao ambao pia wakaingia bafuni mle wakijifanya nyuso zao kumbe walizuga tu, lengo kuu ilikuwa kumtazama Eddy...

SONGA NAYO UJUE KILICHOJIRI....

. . ..EDDY aliendelea kuoga bila kujua kuna watu wanapiga chabo mle bafuni. Alijua wanafunzi wale wanamtazama kwa wema tu au labda wanautazama uzuri wake aliojaaliwa na Mwenyezi Mungu ambao daima unawachanganya mabinti na hata wanawake watu wazima ambao kuna wakati walimrubuni kwa kumpa vitu vya thamani ili awakubalie lakini bado hawakumpata kijana yule kutoka kwenye familia ya kitajiri ya Mr.Alloyce.

Eddy aliendelea kuoga kwa kujiamini mpaka alipofikisha mkono kwenye maeneo yake nyeti. Ghafla alishtuka sana kama vile amepigwa shoti ya umeme, macho yalimtoka kama MTU aliyekutana na simba USO kwa USO porini.

Eddy hakuamini alichokihisi, akaamua kuyapeleka macho yake moja kwa moja mpaka kwenye bustani yake muhimu. Akagundua kuwa sehemu zake za siri hazipo. Bado Eddy hakuamini akachukua maji kwenye kiganja chake cha mkono na kuyasafisha vizuri kwani alihisi hayaoni vizuri. Jibu likabaki moja tu Sehemu zake nyeti hazikuwepo.

"What! Mbona sielewi!" Eddy alichanganyikiwa kupita kiasi. Akachukua suruali yake na kuivaa kwa wizi ili watu wasimwone lakini alikuwa tayari amechelewa kwani alikuwa tayari ameshaonwa na watu wengi tu.

Bila hata kujiosha povu la sabuni alilokuwa amejipaka mwilini, Eddy alikimbia na kuingia bwenini. Akajibwaga kitandani kwa Jackson rafiki yake bila kujali kuwa sabuni iliyoko mwilini mwake ilichafua shuka.

"Eddy! Vipi mshkaji!" Aliuliza Jackson huku akimalizia kuvaa sare zake za shule.

" Nakufa Jack... Nakufa Mimi...."

" Unakufa? Mbona sikuelewi Eddy?" Jackson alikuwa haelewi chochote kinachoendelea kuhusu Eddy ingawa taarifa zilikuwa zimesambaa kwa wanafunzi wengi wa kiume.

" Eddy! Niambie umepatwa na nini? Unaniacha njia panda.."

" Jack... Nakufa... Siwezi kuishi... Nakufa..." Eddy alizidi kulia kama mtoto mdogo aliyenyimwa maziwa kwa muda mrefu. Akili yake haikufikiria kingine zaidi ya kujiua, asingeweza kuistahimil aibu ambayo ilimjia kwa kasi bila hata kupiga hodi.

"Jack..Dunia hadaa ulimwengu shujaa.. Jack me nakufa.. Waambie wazazi wangu..Nilipenda visivyopendeka ila sio kwa matakwa yangu naamini ni shetani tu.."

Maneno hayo yaliibua simanzi nzito kwa Jackson, machozi yalimzidi nguvu hivyo yakashuka kwa kasi machoni kwa Jackson.

"Hapana Eddy huwezi kufa, hebu niambie tatizo..!"

"Hata nikikwambia huwezi kunisaidia Jack.. Huwezi amini natamani kuwa hata nyuki wa mashineni kwa sasa!"

" una maana gani!"

"Mimi sio mwanaume tena... Unafikiri nitaificha vipi aibu hii? Bora nife.. Nikapumzike na wafu wenzangu.."

"Eddy! Sio mwanaume tena kivipi?"

"Uume wangu haupo!" Eddy aliposema hayo akashindwa kujizuia kulia kwa sauti. Hivyo akalia kwa sauti Kali iliyosikika bweni zima. Kwa bahati nzuri wanafunzi karibia wote walikuwa wameondoka ili wawahi mstarini.

Jackson alitazama SAA yake ya mkononi ilikuwa tayari SAA mbili kasoro.

" Eddy! Nitarudi sasa hivi ngoja nikakuombee ruhusa kuwa unaumwa, ila please usifanye lolote. Niahidi!"

Eddy aliitikia kwa kichwa kuwa hatofanya lolote, Jackson akatoka huku akiwa na wasiwasi sana.Eddy aliona dunia inamwelemea na ni vigumu kukabiliana nayo. Machozi hayakuacha kumtiririka kila sekunde. Akili yake ikaanza kukumbuka mambo mengi, ndipo alipoupata ukweli kuwa Doreen ndiye aliyemfanyia ukatili ule Jana usiku.

Akili ya Eddy ikawa kama imefunguliwa kutoka kwenye kifungo kikali. Akamkumbuka Dorice wake, msichana ampendaye sana kuliko mwingine yeyote ila akakumbuka kuwa alishamsaliti na kumdhalilisha mbele za watu.

"U wapi Dorice mpenzi wangu! Dorice nisamehe ! Dorice haikuwa akili yangu! Nakupenda Dorice! Ingawa nakufa ila naomba unisamehe sana.... Doreen ni shetani! Hafai hata kidogo..!" Eddy alilia mpaka kamasi zilimtoka. Kichwa kikamgonga kutokana na kulia kwa muda mrefu.

Eddy aliinuka kitandani pale na kwenda moja kwa moja kwenye begi lake. Akachukua kijidaftari kidogo, akachana karatasi ndogo. Kisha akachukua kalamu akaanza kuandika ujumbe huku machozi yakililowanisha karatasi lile .

" Dorice mpenzi, nisamehe kwa yote yaliyotokea Nakupenda sana. Halikuwa kusudio langu mpaka sasa sielewi ilitokeaje. Mpaka kaburini, kumbuka upendo wangu, ujue kwamba Nakupenda! Nakufa mpenzi ila bado nakupenda!"

Eddy alimaliza kuandika ujumbe huo wa kusikitisha kisha akalikunja karatasi lile na kuliweka kitandani.Eddy alishusha suruali na kujiangalia tens sehemu zake za siri ili ahakikishe kama ni kweli. Ndio ilikuwa kweli kabisa wala so ndoto. Kilio cha Eddy kikaongezeka alishindwa kuvumilia akaona ni heri ajiondoe duniani mapema.

Eddy alifungua begi lake na kuchukua vidonge vingi alivyokuwa akivitumia kwa maumivu ya tumbo, akatafuta vidonge aina nyingine akavichanganya kwa pamoja. Lengo lake ilikuwa avitumie kama sumu ili aondokane na adha zinazomkàbili duniani. Akachukua maji yaliyokuwa kwenye kopo akalisogeza karibu. Akasali sala ya mwisho ili apokelewe vyema na malaika wa huko aendako.