Huenda Miss Tanzania wa zamani, Happiness Millen Magese siku za usoni kama Mungu akipenda akawa na furaha kama ya wanawake wengi duniani – furaha ya kupata mtoto.
Ni kwasababu tatizo lake la Endometriosis limemuondolea matumaini ya kuwa mama lakini sasa inaonekana kuwa matumaini yamerejea, shukrani kwa sayansi ya IVF.
Kwa mujibu wa post aliyoiweka Instagram, huenda Millen akawa amefanyiwa mchakato huo May 13 na hivyo siku za usoni anatarajiwa kuwa mama.
“Sijawa mama tayari lakini ninakikumbatia kila kitu kilichoongezwa kwenye mwili wangu na kwenye maisha yangu kwa ujumla tangu May 13,” inasomeka sehemu ya post aliyoiweka inayomuonesha kwenye video akitembea kwa furaha kwenye ufukwe wa bahari.
IVF ni nini ?
IVF ni njia ya kupandikiza yai na mbegu za kiume iliyogunduliwa miaka 30 iliyopita kama njia ya kuwasaidia wanawake walioharibikiwa na njia ya uzazi kiasi cha kushindwa kushika ujauzito kwa njia ya kawaida.
Mchakato huu huanza kwa mwanamke kuwekea hormonie ili kuamsha uzalishaji seli kwenye nyumba ya yai.
Hizi huchukuliwa kama mayai na kuweka kwenye chombo maalum (test tube) kutengeneza
Embryos (hatua ya kwanza ya kiumbe).
Baada ya siku mbili au tano, embryos hizi huingia kupitia ukeni kwa mwanamke hadi kwenye mfuko wa uzazi ambako mtoto hutokea na miamba hutungwa.
Hata hivyo, kwenye IVF tofauti na njia ya kawaida ya uzazi, sio kila embryo huwa mimba na ndio maana embryo za ziada hutunzwa ili upandikizaji mwingine unaweza kufanyika kama wa kwanza ukifeli.
Wapo mastaa kibao waliowahi kupata watoto kwa njia hii wakiwemo Celine Dion, Mariah Carey, na Nicole Kidman.
-bongo5