SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 7 Julai 2016

T media news

MAZANDA: NIMEANZA MAZOEZI ‘MDOGO-MDOGO’

Na Baraka Mbolembole

KIUNGO ‘maestro’ Steven Mazanda ameanza mazoezi baada ya kusumbuliwa na maumivu ya muda mrefu. Mchezaji huyo wa Mbeya City FC amekuwa na maumivu ya enka na goti ambayo yalichangia akashindwa kucheza sehemu kubwa ya msimu uliopita.

“Nimshukuru Mungu nimeanza mazoezi ‘mdogomdogo’. Kwa kiasi kikubwa maumivu yamekata. Ila sitaki kufanya haraka. Naenda na ushauri wa madokta ila nitapona kabisa. Tatizo nilicheza muda mrefu na maumivu bila kujali kwamba naongeza tatizo. Anasema Mazanda nilipofanya naye mahojiano mafupi siku ya Jumatano hii.

Picha zote kwa hisani ya www.mbeya city fc.co.tz