Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyopewa amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali, na pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
Mhe. Augustino Lyatonga Mrema.
Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2016.
Mhe. Augustino Lyatonga Mrema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Mhe. Eusebia Nicholaus Munuo ambaye muda wake umemalizika.
Prof. William R. Mahalu
Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.
Prof. Mohamed Janabi
Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Prof. Angelo Mtitu Mapunda
Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Bi. Sengiro Mulebya
Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Bw. Oliva Joseph Mhaiki
Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Mwl. Winifrida Gaspar Rutaindurwa
Ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Dkt. Charles Rukiko Majinge
Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.
Dkt. Julius David Mwaiselage
Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Kupandishwa Vyeo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 25 wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP).
Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;
Essaka Ndege MugasaAdamson Afwilile MponiCharles Ndalahwa Julius KenyelaRichard Malika RevocatusGeofrey Yesaya KamwelaLucas John MkondyaJohn Mondoka GudabaMatanga Renatus MbushiFrasser Rweyemamu KashaiFerdinand Elias MtuiGermanus Yotham MuhumeFulgence Clemence NgonyaniModestus Gasper LyimoMboje John Shadrack KangaGabriel G.A. NjauAhmed Zahor MsangiAnthony Jonas RutashubulugukwaDhahir Athuman KidavashariNdalo Nicholus ShihangoShaaban Mrai HikiSimon Thomas ChilleryLeonard Lwabuzara PaulAhmada Abdalla KhamisAziz Juma MohamedJuma Yussuf AllyAidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi wengine 34 kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;Fortunatus Media MusilimuGoyayi Mabula GoyayiGabriel Joseph MukunguAlly Omary AllyEdward Selestine BukombeSifael Anase MkonyiNaftari J. MantambaOnesmo Manase LyangaPaul Tresphory KasabagoDadid Mshahara HizaRobert MayalaLazaro Benedict MambosasaCamilius M. WamburaMihayo Kagoro MsikhelaRamadhani Athumani MungiHenry Mwaibambe SikokiRenata Michael MzingaSuzan Salome KagandaNeema M. MwangaMponjoli LotsonBenedict Michael WakulyambaWilbroad William MtafungwaGemini Sebastian MushiPeter Charles KakambaRamadhan Ng'anzi HassanChristopher Cyprian FuimeCharles Philip UlayaGilles Bilabaye MurotoMwamini Marco LwantaleAllute Yusufu MakitaKheriyangu Mgeni KhamisNassor Ali MohammedSalehe Mohamed SaleheMohamed Sheikhan MohamedMaafisa hawa wa Jeshi la Polisi Tanzania wamepandishwa vyeo kuanzia tarehe 15 Julai, 2016.