Mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz kutoka Tanzania ametajwa kuwa msanii pekee kutoka upande wa Afrika Mashariki kupanda kwenye stage ya tamasha la Afrika litalofanyika New York July 22.
Ni tamasha ambalo kwa mara ya kwanza litafanyika kwenye ukumbi wa Barclays Centre, ukumbi ambao Wamarekani wamezoea kuona mastaa wakubwa wakitumbuiza hapo kama Jay Z.
Ni ukumbi ambao unaweza kuchukua watu mpaka elfu 20 ambapo Diamond ameonekana mwanamashariki pekee huku wengine wakiwa ni Wanigeria kama Davido, Wizkid naIyanya.
Diamond akuletea muziki zake kupitia Wasafi Classic Baby kwenye MzookaJumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.
Hii ni mara ya kwanza kufanyika kwa tamasha hilo kubwa nchini Marekani, siku zote wasanii wa Afrika wamekua wakitumbuiza hapa lakini hawaingii kwenye kumbi zinazochukua watu wengi kama hivyo.
Waandaaji wa tamasha hilo wameiambia DStv kwamba imewachukua miaka mitatu kuaminika na kupewa sehemu ya kufanyia tamasha hilo, kilichokua tatizo sio pesa, ni kuaminiwa na kupewa hiyo sehemu kufanyia tamasha.
Matangazo ya tamasha hili kubwa yanasikika kwenye vituo vya redio maarufu New York Marekani ikiwemo Hot 97 pamoja na Power 105.1.