SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 6 Aprili 2016

T media news

RIPOTI MPYA YA ASKARI WA TZ WALIOHUSISHWA NA KASHFA YA NGONO CONGO



Mkuki ni mtamu kwa nguruwe ila kwa binadamu ni mchungu  ndivyo itakavyokuwa kwa wanajeshi wa tanzania ambao waliwapa “mimba” wananwake huko nchini DRC na sasa ni zamu yao kuchunguzwa na huenda kawatiwa hatiani kwani baadhi walifanya mapenzi na wasichana chini ya miaka 18 ambapo kwa hapa kwetu Tanzania ni kosa la jinai..

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema Tanzania imeshaandaa timu ya uchunguzi ambayo itasafiri kwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kuchunguza madai kuwa askari wake walio katika kikosi cha Umoja wa Mataifa walihusika na unyanyasaji wa kingono.

Farhan Haq amesema Ujumbe wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa mjini New York umetangaza uamuzi huo baada ya kikao na Idara ya Usaidizi kwa ajili ya vitengo vya Umoja wa Mataifa katika nchi mbalimbali. Haq amesema Umoja wa Mataifa unaishauri Tanzania kuendesha uchunguzi huo kwa ushirikiano na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Usimamizi wa masuala ya ndani (OIOS).

Haq ameongeza kwamba miongoni mwa wanawake 11 wanaodaiwa kuwa wahanga wa ukatili huo wa askari Watanzania, sita walikuwa wenye umri wa chini ya miaka 18.

Aidha ameeleza zaidi kwamba saba wameshajifungua na wengine wanne bado wako na ujauzito, na kwamba wote sasa hivi wanasaidiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF ambalo limetuma timu maalum kwa ajili yao.

Askari wote wa kikosi cha Tanzania nchini DRC wamezuiliwa kambini huku uchunguzi ukiendelea. Vitendo hivyo vyote vimeripotiwa katika kijiji cha Mavivi mashariki mwa DRC karibu na Beni. Umoja wa Mataifa una askari elfu 18 katika kikosi chake cha kulinda amani DRC

Askari wa Umoja wa Mataifa kote duniani wamekumbwa na kashfa za ubakaji , Tuhuma hizo zilitangazwa Jumatatu hii na msemaji wa Umoja wa Mataifa.