SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 9 Aprili 2016

T media news

VYAKULA VINAVYOONDOA SUMU MWILINI


Image result for chakula kinacho ondoa sumu
                                                                       



Njia  nzuri inayoweza kutusaidia kuondoa sumu na hasa zile zinazozalishwa mwilini ni matumizi ya vyakula bora, hivi ni vyakula ambavyo kwa asili yake huwa na virutubisho ambavyo huvunja vunja na kuondoa sumu mwilini, vyakula hivi kitaalamu huwa na vitu vinavyoitwa antioxidants, ambavyo huulinda mwili dhidi ya kemikali hatarishi zinazozalishwa mwilini. Virutubisho hivi ni pamoja na


 Image result for chakula kinacho ondoa sumu                                                                   



Vitamin A, Vitamini C na Vitamini E. Vitamini hizi hupatikana katika mboga za majani na matunda, mfano mchicha, spinachi, karoti, matembele, machungwa, nanasi, maembe, machenza pamoja na mafuta ya mimea mfano alizeti.Ili miili yetu iweze kufanya kazi vizuri na tuendelee kuwa na afya njema, inabidi tuepukane na sumu hizi, pale inapo tulazimu zitumike (mfano zebaki, migodini), basi tuzidishe umakini katika kujilinda afya zetu, na pia tubadilishe aina ya maisha au ulaji wa vyakula, matunda na mboga za majani ni walinzi wakubwa sana wa afya zetu.