SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 8 Aprili 2016

T media news

Ndizi na maajabu yake katika matibabu


NDIZI ni miongoni mwa tunda lenye ladha nzuri na hupendwa na watu wengi katika nchi mbalimbali hapa ulimwenguni ikiwemo Tanzania,.

Ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalam kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’ na vile vile ina kiasi kingi cha nyuzi yaani 'fiber' ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.

Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili, ambapo pindi ulapo tunda hili unaweza kupata nguvu ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakuwa umekula ndizi mbili tu na kwa sifa hiyo tunaweza kusema ndizi huenda likawa tunda muhimu sana pia kwa wanamichezo.

Hata hivyo, nishati siyo faida pekee unayoweza kuipata katika ndizi kwani pia ni tunda lenye uwezo wa kuponya na kuzuia matatizo mengine ya kiafya likiwemo suala la mfadhaiko wa akili (depression)

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama cha Afya ya Akili cha Taifa (MINDI) cha nchini Uingereza kwa watu wanaosumbuliwa na tatizo la mfadhaiko wa akili, watu wengi waliondokana na tatizo hilo na kujisikia vizuri baada ya kula ndizi mbivu. Hali hii inatokana na ukweli kwamba ndizi huwa na kirutubisho kinachojulikana kama ‘tryptophan,’ ambacho ni aina fulani ya protini inayotumika mwilini kumfanya mtu kuwa mtulivu na mwenye furaha.

Hali kadhalika, ndizi pia huwasaidia wanawake wanaopata matatizo wakati wa hedhi, hivyo endapo wewe ni miongoni mwa wale akina mama wanaopatwa na matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa hedhi, unashauriwa kula ndizi mbivu na unaweza kuponywa.

Mbali na kusaidia wakina mama katika matatizo ya hedhi pia ndizi huweza kuwasaidia watu ambao husumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu (anemia), hii ni kwasababu ndizi imekuwa ni chanzo kizuri cha madini ya chuma (iron), hivyo inaweza kuwa ni dawa ya kuzuia na kuponya tatizo la upungufu wa damu kwasababu madini ya chuma huamsha uzalishaji wa chembechembe za damu mwilini.

Sambamba na faida hizo za tunda hili pia inaelezwa huweza kusaidia kupunguza kasumba ya 'hangovers' ndizi ni moja ya dawa ya haraka ya kuondoa uchovu unaotokana na ulevi wa jana yake (hangovers) , hivyo unaweza kunywa ‘milk shake’ iliyotengenezwa kwa ndizi na kutiwa asali.

Hali kadhalika ndizi hutuliza tumbo ikiwa itsaidiwa na asali, inayorejesha kiwango cha sukari kilichopungua kwenye damu wakati maziwa nayo hutuliza na kurejesha maji kwenye mfumo wake.

Pamoja na hayo, ndizi pia husaidia katika matatizo mengi na kutuliza mishipa ya fahamu, kuondoa wasi wasi, kutuliza vidonda vya tumbo, tindikali na kushusha joto la mwilini pamoja na kurekebisha mapigo ya moyo. n.k.

Lakini pia kwa wale wenye kupatwa na majeraha yatokanayo na kuungua kwa moto huweza kujitibu kwa kutumia ndizi badala ya kutumia asali pekee ambayo kuna wakati huweza kuwa inapatikana mbali na eneo ulipo kwa wakati huo. Namna ya kutumia hii ni kupondaponda ndizi iliyoiva vizuri kisha tumia rojo hilo la ndizi kwa kupaka sehemu iliyoungua halafu bandika jani la mgomba kama bandeji kisha endelea na tiba hiyo hadi kidonda kitakapopona.

Pia ndizi huweza kumaliza tatizo la ukavu wa ngozi, ambalo huchangiwa na hali ya joto kali au mtu mwenye tatizo la kutapika tapika mara kwa mara au kuharisha huweza kukumbwa na tatizo hili.

Hivyo, ili kukabilia na tatizo hilo, ndizi nayo ni muhimu sana kwa mtu mwenye tatizo hili la kupauka kwa ngozi, hii ni kwa sababu tatizo hilo huchangiwa na ukosefu wa madini mbalimbali hasa yale ya ‘potassium’ ndani ya mwili, hivyo ndizi huwa na madini hayo ambayo husaidia kurejeshesha unyevunyevu kwenye ngozi, lakini pia tatizo hilo huweza kudhibitiwa kwa kunywa maji mengi zaidi.