SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 4 Aprili 2016

T media news

Bifu la Wanamuziki Diamond Platnumz na Ali Kiba Sasa ni Vita ya Kifamilia!


Imevuja! Harakati za kusaka mafanikio na kufika mbali kimuziki zimeibua jipya kati ya wakali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ ambapo vita yao imehama kutoka kwa mtu na mtu na sasa imekuwa ya kifamilia.

Wachunguzi wa masuala ya burudani Bongo wanadai kwamba, kila mmoja anatumia familia yake kujifanyia matangazo (promo).Kwa mujibu wa sosi aliye karibu na Kiba, kwa sasa jamaa huyo anatembelea nyota au Waswahili wanasema viatu vya Diamond kwa kufuata staili ileile anayoitumia kujifanyia promo ambayo mpaka sasa imempa mafanikio makubwa.

KISIKIE CHANZO
“Hivi Wikienda mnajua kuwa kwa sasa Ali (Kiba) ameona afuate staili ya Diamond? Kwa sababu kama ninyi ni wafuatiliaji mtagundua kuwa zamani alikuwa hana mazoea ya kuanika familia yake kama ilivyo sasa.

AANISHA STAILI HIYO
“Kwa mfano ni hii staili yake mpya ya kutoka na mama, dada yake, Zabibu na sasa anatumia hata watoto kama Diamond anavyomtumia Tiffah (Latifah Nasibu).

“Hii ni staili ambayo amekuwa akiitumia Diamond ambaye huwa anapenda kutoka na Esma (Platnumz) au Queen (Darleen) na mama yao, Sandra (Sanura Kassim) kisha anamuongezea Zari

UHUSIANO NAO WATAJWA
“Kiukweli kabla ya Diamond kuwa anafanya hivyo, zamani Kiba tulikuwa hatumuoni anaonesha uhusiano wake na mwanamke hadi ana watoto watatu kwa mama tofauti lakini hata siku moja, hakuwahi kuwaonesha mama zao kwa maana ya uhusiano alikuwa akifanya siri.

AANIKA UHUSIANO WAKE NA JOKATE
“Kuonesha kuwa anakanyaga viatu vya Dangote (Diamond), alivyoingia kwenye uhusiano na Kidoti (Jokate Mwegelo), akaanza kujiweka wazi kama Diamond huku habari zake zikitawala kwenye media (vyombo vya habari) mbalimbali ndipo akaanza kushaini,” kilisema chanzo hicho na kuweka pozi kidogo.

MAMA ADAIWA KUTOA KIAPO
Chanzo hicho kiliendelea kunyetisha kuwa, Mama Kiba amekula kiapo cha kuhakikisha anamtoa mwanaye kama ilivyo Mama Diamond na kuahidi kuwa naye kwenye kila jambo atakalokuwa akilifanya kuhakikisha anampaisha mwanaye.

Kilitambaa na mistari kuwa, Mama Kiba anajua busara za mama humuongoza mtoto hivyo kwa sasa hataki kukaa mbali hivyo atafanya kila njia kuhakikisha mwanaye anakuwa juu.

KIBA AANGUSHA PATI YA MWANAYE AMAYA
‘Ubuyu’ ulizidi kumwagwa kwamba, katika kuonesha kuwa kwa sasa ameamua, hivi karibuni Kiba alimfanyia mwanaye, Amaya bonge la pati ya ‘bethidei’ akionekana akikata keki na kuruhusu mapichapicha tofauti na zamani ambapo alifanya mambo yake kwa usiri mkubwa.

DIAMOND MBELE KWA MBELE
Chanzo kingine cha upande wa Diamond kilieleza kuwa wakati Kiba akimfukuzia jamaa huyo kwa kufuata nyayo zake, msanii huyo naye ameongeza spidi ili kuzidi kufika mbali.

“Sasa hivi vita ni ya kifamilia zaidi, yaani Diamond ndiyo anazidi kuongeza familia ya Wasafi ili kila mmoja atumie fursa ya kumtangaza afike mbali zaidi,” kilisema chanzo hicho.
diamondplatnumzMondi akiwa na mamaake.


Baada ya kunyetishiwa habari hiyo, Wikienda lilimwendea hewani Kiba ili kupata ukweli wa kile kinachoelezwa ambapo mambo yalikuwa hivi;
Wikienda: Kiba mambo vipi? Nina maswali nataka kukuuliza maana kuna shabiki wako ametunyetishia ubuyu f’lani hivi.
Kiba: Hakuna shida ongea tu.

Wikienda: Kuna madai kuwa wewe kwa sasa unafuata staili ya Diamond kwa kuamua kumuanika mama yako kila kona, unalizunguziaje hili?
Kiba: Siyo kweli. Mama yangu aliniomba aje kwenye event yangu ndiyo maana nilimkubalia.
Wikienda: Mbona inadaiwa kuwa umeona ndiyo njia ya kukupaisha kwani zamani ulikuwa huna kawaida ya kuanika uhusiano wako wakati wa Jokate umemwanika kwa sababu ya kutafuta kiki?
Kiba: Ehee, endelea..
Wikienda: Samahani hivi wewe una baba?
Kiba: Ninaye ndiyo, yupo nyumbani Kariakoo (Dar). Kwani vipi?
Wikienda: Mbona hujawahi kumuanika kwa mashabiki wako?
Kiba: Siyo kweli, alishaonekana, kuna wakati waandishi walinifuata nyumbani nikapiga naye picha na naomba niseme tu mimi kuonekana na wazazi wangu siyo lazima, inategemea na ishu, kama ishu itakuwa ni lazima wazazi waonekane, wataonekana lakini kama haina ulazima hawataonekana.

DIAMOND VIPI?
Alipotafutwa kuhusiana na ishu ya vita yao ya mafanikio kuwa sasa inahusisha familia, Diamond alifunguka:

“Kila mtu ana namna yake ya kutoboa ‘so’ siyo mbaya mtu ukitumia fursa zote zilizopo, mimi sasa hivi kuna vitu vipya kibao, hapa (Paris, Ufaransa) nimekutana na Fally (Ipupa) na Awilo (Longomba) na tayari mtoto wa Kimanyema nimeshafanya kweli,” alisema Diamond.

DIMOND NA KIBA
Diamond na Kiba wamekuwa kwenye vita kubwa ya kutafuta mafanikio ya kimuziki kwa muda mrefu ambapo wachambuzi wa burudani wanaitafsiri kuwa imechangia kuwasukuma mbele lakini imewagawa mashabiki wao.

Chanzo:GPL