Baada ya msanii wa muziki kutoka ‘label’ ya WCB, Harmonize kudai Rich Mavoko tayari ni member wa label hiyo, Rich Mavoko aibuka na kuzungumzia swala hiyo.
Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii, Rich amedai bado yeye ni msanii huru.
Pia Mavoko ameeleza nini kinamchelewesha kusaini kwenye label hiyo.
Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii, Rich amedai bado yeye ni msanii huru.
“Hizi stori nimezisikia kama Harmonize alivyosema, hii issue imetokea kwa sababu aliniona na Salam (Meneja na Diamond) na tulikuwa tunaongea issue nyingine, atakuwa hajaelewa nini kinaendelea na siwezi kumlaumu sana. Lakini sijui kusema nipo official hapana bado, kama ikiwa official kwanini niwafiche?, haya ni maisha ya mtu na hii ni biashara,” alisema Rich Mavoko.Aliongeza, “Tunapokuja kwenye swala kama hili ni lazima niangalie kama kuna faida ua hasara. Kwa hiyo kitu kikubwa ndio hicho Harmonize aliniona na Salam na simlaumu kwa sababu hajui chochote, kama itakuwa official lazima nitasema kila mtu ajue,”
Pia Mavoko ameeleza nini kinamchelewesha kusaini kwenye label hiyo.
“Hili swala tatizo linazungumza sana mitaani, lakini mimi binafsi nisema vitu vitakapo kuwa tayari mimi nitaweka wazi na kama ikishindikana pia nitasema, lakini kwa sasa kuna mambo yanaendelea,” alisema Rich.