SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 8 Machi 2016

T media news

Nguvu za kiume ni nini


Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi kubwa sana.

Katika kilele cha mwisho kabisa cha furaha katika maisha ya ndoa, kama inavyofahamika, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa. Hata hivyo, ili furaha ipatikane ni lazima tendo lenyewe lifanyike katika hali ya afya kwa wanandoa.

Nguvu za kiume ni istilahi inayotumika mara nyingi kurejelea ‘uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa kinyume chake, tunasema ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’. Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana. Inaweza kuwa ni kujumuisha hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.

Licha ya hivyo, elimu mhimu kabisa ambayo mwanaume anapaswa kuifahamu ni kuwa, nguvu hizi hazitoki katika madawa ya kemikali au pahala pengine; zinatoka katika vyakula tu.

Kushindwa kwa uume kusimama pia hujulikana kama kuishiwa nguvu za kiume. Ni kitendo cha mtu kushindwa kusimamisha uume au kudumisha usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la tendo na mwenzake. Lakini wakati hii inaweza kumfikisha mwanaume katika upeo wa raha (orgasm), hali hii humwacha mwanamke akiwa hakuridhika. Mke wako hukutaka ukawie ikiwezekana ukawie zaidi. Kama mwanaume hataweza kukawia, basi anakuwa hampi raha mke wake.

Hata hivyo, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako. Takribani asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wana tatizo hili. Lakini vile vile kufahamu tu kuwa wanaume wengine pia wana tatizo kama lako haitakusaidia kuondoa shida inayokukabili.

Kuna wakati kushindwa kusimama uume kunaweza kuonekana kama si tatizo lakini wakati hali hiyo inapoendelea kwa muda mrefu inaweza kuleta hisia ya dhiki kubwa kwa mme na mke wake.