SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 19 Machi 2016

T media news

Mwanamuziki Shaa Achukizwa Vibaya na Bifu ya Ali Kiba na Diamond Platnumz...Adai Inamuweka Katika Wakati Mgumu Sana


Shaa amekiri kuwa hakuna beef asiyoipenda kama ya Diamond na Alikiba.
Amesema inawaweka wasanii wengine pia katika wakati mgumu.
“Ni sababu Alikiba ni msanii ambaye nampenda hatari, halafu Diamond ni msanii ambaye namkubali hatari,” amesema Shaa.
“Kwahiyo mnaniweka kwenye wakati mgumu hata mimi mwenyewe shabiki wote wawili nawapenda, wote wawili nawakubali lakini mmevuruga issue to a point ambayo siyo. Yaani Alikiba ni njano, halafu Diamond ni kijani, halafu nyie mmevuruga mechi yaani mimi sipendi kabisa kusema ukweli,” ameongeza.
“It’s allowed kupenda wasanii wote at the same time lakini watu wa media unfortunately ndiyo mnatuweka kwenye wakati mgumu.”