Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.
Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen’genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.
Historia inaonesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika China mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Roma. Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana.
Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia. Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii ya vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash).
Huko sokoni tayari nimeviona vitunguu swaumu kutoka China na Afrika kusini ambavyo vyenyewe huwa vina punje kubwa nene na huwa rahisi kuvimenya, hata hivyo ili upate faida hizi zote hapa chini naendelea kukushauri utumie vitunguu swaumu vyetu vinavyolimwa hapa Tanzania kwani hivyo vya kutoka nje pamoja na kuwa ni rahisi kuvimenya lakini ubora wake si kama ule wa vitunguu vyetu.
Hakikisha kila mboga unayopika haikosi kitunguu swaumu ndani yake na ikibidi ukiweke mwishoni mwishoni unapokaribia kuipuwa mboga yako toka katika moto kwamba kisiive sana hata kupoteza viinilishe vyake. Kama una friza au friji ya kawaida unaweza kumenya vitunguu swaumu hata kilo nzima na kuvitwanga kidogo katika kinu, vifunge vizuri katika bakuli au mfuko wa plastiki na uvihifadhi katika friza au friji na hivyo kila unapopika unachukuwa tu na kukitumia ili kuepuka usumbufu wa kukimenya kila siku.
Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.
Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
Kigawanyishe katika punje punje
Menya nusu yake (punje 8 au 10 hivi),
Menya punje moja baada ya nyingine
Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu
Meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala au fanya kutwa mara 2 kama unaumwa na moja wapo ya magonjwa niliyoyaorodhesha hapa chini.
Fanya hivi kila siku au kila mara unapopata nafasi na hivyo utakuwa mbali na kuuguwauguwa. Mama mjamzito chini ya miezi 4 ni vema asitumie, kwa ujumla tu mjamzito uwe makini utakapotumia kitunguu swaumu kwa namna hii kama wewe ni mjamzito.
Kitunguu swaumu hutibu magonjwa 30
Haya ni baadhi ya magonjwa yanayotibika au kukingika na kitunguu swaumu:- Huondoa sumu mwilini
- Husafisha tumbo
- Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro)
- Husafisha njia ya mkojo
- Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria
- Huzuia kuhara damu (Dysentery)
- Huondoa Gesi tumboni
- Hutibu msokoto wa tumbo
- Hutibu Typhoid
- Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi
- Hutibu mafua na malaria
- Hutibu kifua kikuu
- Hutibu kipindupindu
- Hutibu upele
- Huvunjavunja mawe katika figo
- Hutibu mba kichwani
- Huupa nguvu ubongo
- Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu
- Huongeza SANA nguvu za kiume
- Hutibu maumivu ya kichwa
- Hutibu kizunguzungu
- Hutibu shinikizo la juu la damu
- Huzuia saratani/kansa
- Hutibu maumivu ya jongo/gout
- Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
- Huongeza hamu ya kula
- Huzuia damu kuganda
- Husaidia kutibu kisukari
- Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi
- Huongeza SANA kinga ya mwili
- Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
- Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
- Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
- Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo hutolewa baada ya kuvila.
Nini madhara ya vitunguu swaumu?
Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;
- Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa au kunywa maji mengi.
- Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
- Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha.
- Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.
- Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.
- Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.
Makala nyingine zinazohusiana na hiii:
- Tatizo la Nguvu za Kiume na Suluhisho lake
- Hizi ndizo faida 50 za mazoezi
- Kachumbari/fresh mixed salad
- Tabia 10 zinazoharibu Figo
- Faida 7 za Juisi ya Nyanya
- Faida za majani ya Stafeli
- Jitibu kwa kutumia maji mp3
- Maajabu ya juisi ya Ubuyu
- Kazi 10 zitakazokushangaza za mafuta ya nazi
- Asali na Mdalasini
- Maajabu ya mlonge
- Vidonda vya Tumbo MP3
- Ukweli Kuhusu UKIMWI