SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 11 Machi 2016

T media news

Jinsi ya kutengeneza Halua


Mahitaji
1 kikombe unga wa corn flower/
kikombe  brown sugar
2 vikombe white sugar
3 cup maji

kijiko kimoja cha chai kungu manga
Zafarani kijiko kimoja cha chai
Iliki kijiko kimoja cha chai
Mafuta ya kula vikombe viwili/unaweza tumia samli fresh
Ufuta vijiko vitatu vya chakula
Lozi vijiko 3 vya chakula
Halua inapikwa kwa lisaa limoja

Namna ya kupika
Chukua bakuli kubwa weka sukari zote white na brown,iliki,kungu manga,weka maji,na unga koroga hadi kila kitu kilainike yaani sukari na unga.

Bandika sufiria yako jikoni iwe kubwa kiasi mimina mafuta au samli iache hadi ipate moto sana mimina ule mchanganyiko wako 

Koroga bila ya kupumzika ikifika dk 45 weka ufuta wako/lozi,halafu koroga hadi litimie lisaa limoja.
Hapo Halua yako itaku tayari Paka sinia mafuta mimina Halua yako iache ipoe tayari kwa kuliwa.