Karibu mpenzi msomaji wangu na leo ninakuletea somo hili la namna ya kuandaa juisi safi na yenye afya, juisi ya nyanya. Endelea kusoma …
Unahitaji;
Nyanya kubwa 8
Jira (cumin seeds) vijiko vya chai viwili
Pilipili manga nyeusi ya unga (black pepper powder) robo kijiko cha chai
=> Safisha nyanya vizuri, nyanya zilizoiva vizuri lakini siyo zilizoiva sana.
Iondoe sehemu ya juu ya nyanya (kikonyo), kata vipande vidogo vidogo na utumbukize kwenye blenda, ongeza mbegu za jira na maji kidogo na kisha uzisage kwa pamoja.
Mwishoni ongeza kiasi kidogo cha pilipili manga nyeusi ya unga. Koroga vizuri, chuja na chujio juisi yako, mimina kwenye glasi na Unywe.
Faida 7 za Juisi ya Nyanya
1 . Husaidia kuulinda mwili dhidi ya kolesteroli
2 . Juisi ya nyanya ina kiasi kingi cha vyanzo vya vitamini A na C
3 . Faida nyingine kubwa ya juisi ya nyanya ni uwezo wake katika kukusaidia kupunguza uzito uliozidi mwilini.
4 . Kama kuna juisi nzuri kwa mwili basi ni juisi ya nyanya, na ndiyo maana nyanya ni kiungo kwa karibu kila mboga jikoni.
5 . Juisi ya nyanya pia ina kiasi kingi cha Vitamini B6
6 . Juisi ya nyanya huondoa sumu kwa urahisi zaidi mwilini sababu ina kiasi cha kutosha cha klorine na sulfur
7 . Rangi nyekundu katika nyanya ni matokeo ya kimiminika mafuta kiitwacho ‘lycopene’ ambacho kazi yake kuu ni kuondoa sumu mwilini.