SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 11 Machi 2016

T media news

Dida wa Times FM Aeleza Kisa cha Kutukanwa na Mke Mdogo wa Mzee Yussuf


Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amefunguka na kuzungumzia sababu ya kutukanwa katika mtandao wa kijamii na mke mdogo wa Mzee Yussuf, Chiku.

Mzee Yussuf Jumanne hii aliamua kuwaondoa wake zake wawili Leyla Rashid na Chiku katika mtandao wa Instagram baada ya kuwa wanatupiana maneno machafu kupitia mtandao huo hali ambayo inadaiwa ilikuwa inamchafua mume wao.

Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Dida amedai alitukanwa na Chiku ambaye ni mke mdogo wa Mzee Yussuf kwa madai alikuwa anampendelea mke mkubwa wa Mzee Yussuf, Leyla Rashid.

“Kusema ukweli kila mtu anajua jinsi wake zake Mzee Yussuf, Leyla Rashid na Chiku pamoja na wifi yao walivyokuwa wanarushiana matusi. Lakini mimi kama mimi niliwaHi kuzungumza na Chiku na baadaYe Leyla, lakini nilianza Chiku. Kila mmoja alikuwa anaeleza tatizo nini na kwanini wamekuwa wakitukanana katika mitandao ya kijamii, hawaoni kama wanamuaibisha mume wao! Basi kila mmoja akawa anazungumza kwa pande wake, siku nimezungumza na Leyla akazungumza mambo mengi sana, sasa Chiku baada ya kusikia akawa ananitukana mimi kupitia mitandao,” amesema Dida.

“Mimi binafsi sikumjibu vibaya nikawa namuelewesha nini maana ya uke wenza lakini akawa anaendelea kunitukana. Nikasema Mzee Yussuf ndiye anaweza kumaliza tofauti zao, ngoja nimtafute ili nizungumze naye, akakubali lakini siku ambayo aliniambia nitaongea naye akaniambia amepata dharura na pia hawezi kuja na kuzungumzia mgogoro wa familia yake kwani ataumaliza mwenyewe,” alisema Diva.

Bongo5 ilijaribu kumtafuta Mzee Yussuf ili kuzungumzia suala hilo kwakuwa linamshushia heshima yake, lakini alikataa na kusema tayari ameshafunga ukurasa wa kuzungumzia masuala ya wake zake kwenye vyombo vya habari.

Pia Mzee Yussuf alidai tayari ameshawakataza wake zake kutumia mtandao wa Instagram kwa kuwa ndio chanzo cha ugomvi wao huku na yeye akijipanga kuondoka katika matumizi ya mtandao huo.

Hata hivyo Bongo5 haikuishia hapo, ilizungumza na mtu wa karibu wa Mzee Yussuf ambaye hakutaka kutajwa jina lake na kueleza jinsi mgogoro huo unavyomuumiza kichwa Mzee Yussuf.

“Kweli amewaambia hakuna mtu kutumia mitandao wa Instagram na atakayetumia kwa siri ndiyo talaka yake. Unajua haya mambo huwezi kujua nani ni mkorofi kwa sababu unashangaa tu mambo yamezuka na huwezi kuelewa chanzo chake ni nini. Lakini hii hali inamuumiza sana Mzee kusema kweli, sema watu wa nje wanamchukulia poa,” alisema.