Wakati kukiwa na sintofahamu kuhusu hatma ya uchaguzi wa meya na naibu meya wa Jiji la Dar es Salaam, Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (Alat), imesema kutokamilika kwa mchakato huo hakutaiathiri isifanye uchaguzi wa viongozi wake wapya.
Hayo yalielezwa jana na Katibu Mkuu wa Alat, Habraham Shumumoyo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini hapa.
Shumumoyo alisema kila uchaguzi unafanyika kwa utaratibu wake, hivyo kama wa umeya wa jiji ulikwama kwa sababu fulani, mkwamo huo hauwezi kuwa kizuizi kwao kufanya uchaguzi.
“Kila uchaguzi unaendeshwa kwa utaratibu wake, hata uchaguzi wa uongozi mpya wa Alat tunaufanya kwa kufuata sheria,” alisema na kuongeza: “Kama kuna maeneo hayajakamilisha uchaguzi sisi tunaendelea na ratiba yetu kama ilivyopangwa.”
Katibu mkuu huyo alisema Alat itafanya mkutano mkuu wa uchaguzi wa viongozi wapya watakaoitumikia jumuiya hiyo kwa miaka mitano ijayo mjini Dodoma, Aprili 7 hadi 9, mwaka huu.
Alisema mkutano huo utafunguliwa na Rais John Magufuli na kuwataja viongozi wanaotarajiwa kuchaguliwa na wajumbe wa mkutano huo kuwa ni pamoja na mwenyekiti wa Alat Taifa.
Mwenyekiti huyo anatarajiwa kutoka miongoni mwa wenyeviti wa halmashauri za wilaya, mameya wa halmashauri za miji, manispaa au majiji.
“Wakurugenzi wanne, wawili kutoka halmashauri za wilaya na wawili kutoka halmashauri za miji, manispaa na majiji,” alisema Shamumoyo.
Akizungumzia maandalizi, Shamumoyo alisema yanaendea vizuri. “Lakini bado tunahitaji michango ya wafadhili ili kufanikisha shughuli hii.”
Alisema hadi sasa mfadhili aliyewachangia ni benki ya NMB Sh100 milioni.
Ofisa Mkuu wa wateja wakubwa wa benki hiyo, Richard Mkungwa alisema wametoa mchango huo kwa kutambua umuhimu wa chombo hicho na kazi inazozifanya nchini.