SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 20 Novemba 2016

T media news

Mdau kasafiri kutoka Vikindu ili ashuhudie Sports Extra ikiruka ‘Live’ Mbagala


Watangazaji wa kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM, kutoka kushoto ni Edger Kibwana, Alex Luambano, Issa Maeda na aliyesimama nyuma (mwenye T-shirt ya blue) ni Yahaya Mohamed ‘Mkazuzu’

Malata John Malata ni mdau wa soka ambaye jana alisafiri kutoka Vikindu hadi Sabasaba, Mbagala kwa ajili ya kujumuika na wadau wengine wa soka waliokuwepo Sabasaba Classic Bar kushuhudia game za ligi mbalimbali zilizopigwa Jumamosi ya November 19.

Lakini kubwa zaidi lililomtoa Bw. Malata kutoka Vikindu hadi Mbagala ilikuwa ni kushuhudia show ya Sports Extra ya Clouds FM ikiruka Live kutoka maeneo ya Mbagala-Sabasaba.


Mtangazaji wa Sports Extra Yahaya Mohamed (kushoto) wakati akizungumza na Malata John Malata mdau wa Sports Extra aliyesafiri kutoka Vikindu hadi Mbagala kushuhudia kipindi kikiruka live

Kipindi cha Sports Extra kilirushwa moja kwa moja kutoka Sabasaba Classic Bar ikiwa ni moja ya mikakati ya kipindi hicho kuwafikia wadau wake kwenye maeneo yao ya kujidai, kufahamiana na pamoja na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali yahuyo soka.

Malata alisema alishindwa kujizuia baada ya kusikia kipindi chake anachokipenda kitaruka moja kwa moja kutoka Sabasaba akwahiyo akaona ni fursa ya pekee kwake kushuhudia namna kipindi kinavyoendeshwa pamoja na kuwafahamu watangazaji wa kipindi hicho.

“Kilichonifanya nije hapa ni baada ya kusikia Clouds wapo Sabasaba, nikaona hii ni fursa kwangu kushiriki kwenye kipindi pamoja na kuwafahamu watangazaji wake,” alisema mdau huyo wa soka aliyesafiri kutoka Vikindu hadi Mbagala.

“Mimi ni mkufunzi kwenye Chuo cha Ualimu Vikindu, lakini pia ni mwakilishi wa vilabu wilaya ya Mkuranga na ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya wilaya ya Mkuranga pia ni mjumbe wa mkutano mkuu chama cha soka mkoa wa Pwani (Corefa).”