Mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana ameelezea namna serikali ya mkoa ilivyojipanga kuelekea mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation Cup kati ya Mbao FC dhidi ya Simba itakayofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Dodoma inauzoefu wa kukaribishabwatu kwa makundi makubwa kutoka nje ya maeneo yetu. Kwa hiyo tumejipanga vizuri tunawakaribisha watu kutoka sehemu mbalimbali za nchi nzima tuna hoteli za kutosha wasiwe na wasiwasi.
Tupo kwenye hatua za mwisho kabisa za ukarabati wa uwanja ili uwe salama kwa matumizi ya siku hiyo lakini pia usalama utakuwa wa kutosha ili kila mmoja aweze kuburudika wakati mchezo unaendelea.
Tunawakaribisha Simba, Mbao hata Yanga waje waone kabumbu inavyosakatwa hapa Dodoma na mambo mengine yatakavyokwenda.
Mchezo wa fainali unatarajia kuchezwa Mei 27, 2017 na mshindi wa mchezo huo atakuwa amefuzu moja kwa kucheza michuano ya kombe la shirikicho (Caf Confederation Cup).