SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 18 Novemba 2016

T media news

LINEX AIZUNGUMZIA LEBO YAKE YA VOA KUWA KIMYA

Msanii na msimamizi wa lebo ya Voa Linex a.k.a Sunday Mjeda hatimaye azungumzia sababu inayotufanya tushindwe kuzisikia kazi za wasanii wa lebo hiyo.

Linex ameitaja jina la lebo yake karibu katika nyimbo zake zote alizowahi kuziachia redioni lakini anatuweka wazi sababu ya ukimya huo.

"Kuna kitu kinaitwa VOA na kila kitu lazima kifanyiwe maandalizi ili kiwe kikubwa na kiweze kuingiza pesa pia, sasa ni lazima ukitengenezee mazingira. Mimi nimekuwa brand kwa sababu nime-haso kwa miaka kumi ili kutafuta kitu ambacho ni cha kwangu mwenyewe. Shadoo ndo msanii nimeanza nae na naamini atatoka." Ametusanukia hivyo Linex.

Bongoswaggz itakusongezea stori zote zinazo trend kwenye mitandao ya kijamii na ulimwenguni kote.