SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 29 Julai 2016

T media news

Wanasayansi wagundua dawa kwenye pua ya mwanadamu


Wanasayansi nchini Ujerumani wanasema wamegundua kwamba kuna chembechembe hai kwenye pua ya mwanadamu ambayo inaweza kutumia kuua viini hatari.

Dawa nyingi za kuua viini vinavyosababisha maradhi hutolewa kutoka kwenye wanaoishi kwenye mchanga.

Lakini kutokana na hali kwamba viini vinavyosababisha magonjwa mengi vimeanza kuwa sugu na kutosikia dawa, wanasayansi wamekuwa wakitafuta njia nyingine za kupata dawa mpya.

Ripoti ya vipimo imebaini katika jarida la asili kwamba dawa aina ya Lugdunin, inaweza kutibu maambukizi ya maradhi yasiyosikia dawa.

Watafiti katika chuo kikuu cha Tubingen nchini Ujerumani, waliogundua chembe hizo wanasema kuwa mwili wa binaadamu ni chanzo cha dawa mpya ambazo bado hazijatumiwa.

Dawa ya mwisho kugunduliwa katika mwili wa binadamu ilipatikana mwaka 1980.